SERIKALI KUJENGA NYUMBA 4139 ZA ASKARI POLISI KATIKA MIKOA 17 NCHINI.
SERIKALI
katika mwaka 2016/17 imepanga kujenga nyumba 4139 za askari wa jeshi la
Polisi nchini, hatua itakayosaidia kukabiliana na uchache wa nyumba za
kuishi kwa askari hao.
Awamu ya
kwanza ya nyumba hizo zinatarajiwa kujengwa katika mikoa 17 nchini
ikihusisha mikoa ya Tanzania Bara pamoja na mikoa ya Unguja na Pemba.
Akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Faida Mohammed Bakar, Naibu Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha alisema Serikali
itaendelea kuboresha makazi ya askari na ofisi za polisi kwa awamu kwa
kadri hali ya kiuchumi itavyoimarika.
Ole Nasha alisema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili
askari polisi katika maeneo mbaliombali nchini ikiwemo uchakavu wa
ofisi, ambapo kwa kuanzia imeamua kuanza mpango wa kukarabati ofisi na
makazi ya askari wake.
Aidha
alisema Serikali pia imekusudia kuhakikisha kuwa inatoa mikopo ya vyombo
vya usafiri kwa askari wake ambao wanaishi mbali na vituo vyao vya kazi
ili kuwasaidia kuwahi katika maeneo yao ya kazi kwa wakati.
“Serikali
inatambua changamoto inayowakabili askari wetu nchini ikiwemo wale wa
Kusini Pemba, katika kukabiliana na hali hiyo tumepanga sasa kuifanyaia
ukarabati miundombinu ya ofisi hiyo sambamba na ujenzi wa makazi bora
kwa askari wetu” alisema Ole Nasha.
Katika swali
lake, mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kujenga
nyumba za kuishi Na ofisi za kisasa katika kituo cha mkoani na kengeja
Pemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni