TAA YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA IDARA YAKE YA RASILIMALI WATU
Afisa
Rasilimali Watu Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Fatma
Matimba, akichapa kazi ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wakati wa
kilele cha siku ya Utumishi wa Umma ambapo mwaka huu, maadhimisho hayo
yamefanyika mahala pa kazi ambapo wananchi pamoja na wafanyakazi wa
taasisi husika walipata fursa ya kujipatia elimu ya shughuli mbalimbali
zifanywazo na taasisi husika.
Meneja
Rasilimali Watu Mafunzo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Abdul
Mkwizu (kulia) akimpa maelezo kuhusu mafunzo Ally Zongo, mfanyakazi wa
taasisi hiyo, kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
Afisa
Rasilimali Watu Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Fatma
Matimba (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya upandishaji vyeo kwa
wafanyakazi Omari Hazaa (katikati) na Yusuph Mahadhi (kulia), ikiwa ni
mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2016.
(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni