Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakar asema kesi nyingi zinazofunguliwa Zanzibar hazina mashiko
Na Masanja Mabula –Pemba
MWENYEKITI wa Tume ya
kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakar amesema kuwa kesi
nyingi zinazofunguliwa katika mahakama za Zanzibar hazina mashiko na
zilipaswa kusuluhishwa na jamii kabla ya hazijafikishwa mahakamani .
Amesema kwamba hali hiyo
inasababisha kuwepo na mrundikano wa kesi katika mahakama , kutokana na
jamii kuina mahakama kama sehemu ya kuwasilisha malalamiko hata yale
yasiyo na mashiko .
Jaji Mshibe ameyabainisha hayo
wakati akifungua kikao cha siku moja cha kukusanya maoni juu ya sheria
ya mirathi kwa viongozi wa dini , mahakimu , walemavu pamoja na viongozi
wa kisiasa Kisiwani Pemba katika ukumbi wa Benjemini Mkapa Wete .
Amefahamsha pamoja na kuwepo
kwa vyombo vya ulinziz na viongozi wa serikali za mitaa (masheha) lakini
wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuzuia matendo maovu yasitokea ndani
ya jamii kabla ya kuwafikisha mahakamani .
“Kwa kipindi kimekuwako na
ongezeko kubwa na kesi katika mahakama za Zanzibar na ikizifuatilia
utabaini kwamba hazina mashiko , ambazo zilipaswa kusuluhishwa kabla
hazijafikishwa mahakamani ”alieleza.
Aidha Mshibe alizidi
kufahamisha kwamba kitendo cha jamii kusuluhisha kesi badala ya
kufikishwa mahakamani pia kutaokoa fedha nyingi ambazo zilikuwa zitumike
kwa ajili ya kuandaa shauri hilo .
Alieleza kwamba iwapo kila
mmoja atawajibika kuzuia matukio yasitokee ndani ya jamii , kutaleta
ufanisi wa utendaji wa kazi serikalini kwani watumishi wake hususani wa
mahakama watapunguziwa mzigo wa kupokea mashauri mengi kupita uwezo wa
wa kufanya kazi .
“Kama kila mmoja atawajibika
kuzuia kesi kufikishwa kutaongeza pia ufanisi wa kazi kwa watendaji wa
mahakama zetu , ambao kwa sasa wanapokea kesi nyingi kupita uwezo wa
mahakama zenyewe ”alifahamisha.
Hata hivyo akizungumzia suala
la kuongezwa watendaji wa Idara ya Mahakama , Jaji Mshibe alisema suwala
hilo tayari limepatiwa ufumbuzi , lakini bado changamoto ni jamii
yenyewe kutokuwa tayari kufanya suluhu kwa kesi za kawaida .
Akichangia kwenye kikao hicho ,
Padri wa kanisa la Anglikana Pemba Massoud Emmanuel alisema kwamba ,
bado jamii haijawa tayari kupokea ushauri na maelekezo kutoka kwa
wananchi wa kawaida hata kama utakuwa na maana au faida kwao .
Amesema kwamba viongozi wa dini
wanapowajibika katika kuelimisha jamii , hushushiwa zigo wakidaiwa
kwamba wamekuwa wanasiasa , jambao ambalo linawawia vigumu kuufikisha
ujumbe kwa jamii inayaowzunguka .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni