Watanzania waaswa kuzingatia umri katika kuangalia filamu na maigizo.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fisso akizungumza na
waandishi wa habari ( hawapo pichani) kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo
tasnia ya filamu nchini katika kuazimisha wiki ya Utumishi wa Umma.
————————————————————
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Watanzania wameaswa kuzingatia umri katika kungalia filamu katika majumba ya sinema na sehemu mbalimbali.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar
es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce
Fisso wakati akifafanua masuala mbalimbali kuhusu tasnia ya filamu
nchini kwa waandishi wa habari.
Bibi Joyce Fisso amesema kuwa Bodi
yake inafanya kazi ya kuzipa kiwango kazi za filamu na maigizo ikiwemo
umri sahihi wa kuangalia filamu na hili linapaswa kuzingatiwa na
waoneshaji na waangaliaji wa Filamu.
“ Natoa wito kwa watanzania hasa
wazazi kuzingatia umri katika kuangalia filamu, ukiona imeandikwa umri
wa miaka 18 ujue ni maalum kwa ajili ya umri huo na mtoto chini ya hapo
hatakiwa kuangalia kwasababu maudhui ya filamu au maigizo hayo
hayamuhusu alisisitiza Bibi. Joyce.
Bibi Joyce Fisso ameongeza kuwa
jukumu la kujenga maadili kwa watanzania hasa watoto lipo mikononi mwa
wazazi wao na kuwaasa wazazi kuzingatia umri katika kuangali filamu na
maigizo mbalimbali ili kupunguza wimbi la mmomonyoko wa maadili nchini.
Aidha Bibi Joyce Fisso ameshauri
waandaaji wa filamu na maigizo nchini kuandaa filamu na maagizo yenye
maudhui ya watoto ya kuwajenga katika Mila, Desturi na Tamaduni za
kitanzania kwa kuwa ndio kizazi cha baadae na kinatakiwa kulelewa katika
maadili mema.
Bodi ya Filamu inapokea filamu na
maigizo mbalimbali kwa ajili ya kupata kibali cha kusambazwa na zaidi ya
asilimia 70 ya filamu hizo maudhui yake ni mapenzi hivyo basi jamii
inatahadharishwa kuzingatia umri uliowekwa katika filamu na maigizo hayo
ili kuepukana na mmomonyoko wa maadili kwa watoto uanaozidi kuongezeka
siku hadi siku kwa kuangalia filamu na maigizo yenye maudhui
yasiyowahusu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni