Ijumaa, 1 Julai 2016

Naibu Spika Dkt. Tulia akabidhiwa ripoti ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Bungeni mjini Dodoma

K1 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmbunge wa Nkasi Ali Kessy Bungeni Mjini Dodoma Mapema leo.
K2 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia Bunge Mapema leo mjini Dodoma wakati wa kuhitimisha mkutano wa Tatu wa Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
K3 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akiteta jambo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako Bungeni Mjini Dodoma leo.
K9Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akiongoza ujumbe wa tume hiyo kwenye viwanja vya Bunge leo wakati wa Ziara ya kutembelea Bunge na kuwasilisha ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
K4 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na ujumbe wake uliotembelea Bunge ili kumkabidhi Naibu Spika Ripoti  ya Uchaguzi mkauu wa mwaka 2015.
K5Mwenyekiti wa Tume ya Taifa  ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akikabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Bungeni Mjini Dodoma leo mara baada ya Kuirishwa kwa Bunge.
K6Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akiangalia moja ya vitabu vilivyopo kwenye maktaba ya Bunge wakati wa Ziara ya Mwennyekiti huyo na Ujumbe wake Bungeni mjini Dodoma leo .
K7 
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahamud Hamid akiwa ndani ya maktaba ya Bunge wakati wa Ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.
K8 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ujumbe wake mara baada ya ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma leo.kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva na kulia Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahamud Hamid.
(Picha zote na Frank Mvungi-Dodoma)
———————————————————
Frank Mvungi-Dodoma
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekabidhiwa ripoti ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Bungeni mjini Dodoma leo.
Akizungumza wakati akipokea Ripoti hiyo Naibu Spika amesema kuwa ripoti hiyo ni muhimu kwa Bunge na ni kiashiria cha ushirikiano mzuri kati ya Bunge na Tume hiyo.
“Ushirikiano uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mzuri na kwa upande wangu natumaini tutaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali,” alisisitiza Mhe. Dkt.Tulia.
Akizungumzia majukumu ya Bunge naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia amesema kuwa Bunge la kumi na moja limetimiza majukumu yake vyema  hali itakayochochea  maendeleo hapa nchini katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano      
Kwa upande wake mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tume hiyo na Bunge kama mdau muhimu na kuahidi kuuendeleza kwa maslahi ya pande zote.
Ziara ya Tume hiyo pamoja na kukabidhi ripoti hiyo kwa Naibu Spika ililenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Tume hiyo kuhusu majukumu ya Bunge ambapo wajumbe hao walitembelea maeneo mbalimbali ya Bunge.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ikiwa ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni