Wafanyakazi TBL wahudhuria semina ya malezi ya familia
……………………………………………………………………………………………………..
Katika kuhakikisha wafanyakazi
wake wanapata elimu ya masuala mbalimbali ya kijamii nje ya mazingira ya
kazi,kampuni ya TBL Group imewezesha baadhi ya wafanyakazi wake
kuhudhuria semina ya malezi ya familia iliyofanyika jijini Dar es
Salaam .
Katika semina hiyo wataalamu
mbalimbali wa masuala ya elimu jamii kutoka kampuni ya Grace Inc
walitoa mada kuhusiana na masuala ya malezi bora ya familia na
changamoto zilizopo katika kujenga familia bora ambapo washiriki
walipata fursa ya kuuliza maswali yanaohusiana na malezi ya familia.
Wafanyakazi hao walishukuru
kampuni kwa kuwapatia fursa ya kuhudhuria semina hiyo na walisema kuwa
imewawezesha kupata maarifa mbalimbali yatakayowasaidia kujenga familia
zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni