SHAMBA LA WAZIRI WA SMZ LAVAMIWA NA KUKATWAKATWA NA WATU WASIOJULIKANA
SHAMBA la mikarafuu , minazi
pamoja na mihogo la Waziri asiye na wizara maalumu Zanzibar Said Soud
Said limevamiwa na kuhujumiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia
june 14 mwaka huu .
Katika hujuma hizo zilizotokea
katika shamba lililoko Mgelema Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake ,
jumla ya mikarafuu 29 , minazi 16 pamoja na mashina 250 ya muhogo
yamengo’lewa na baadhi ya mengine kufyekwa na kitu chenye ncha kali .
Katika tukio hilo mikarafuu
michanga 15 imeng’olewa na kutupwa ndani ya shamba , na mengine 14
iliyokuwa tayari kuzaa imekatwa na kuachwa ndani ya shamba .
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi , Said Soud Said alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama
kuhakikisha vinafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliohusika na
vitendo hivyo vya kuhujumu mazao makuu wa uchumi wa nchi .
Aidha alieleza kwamba , baadhi
ya wananchi wanalichukulia suala la siasa kama ni chuki au fitina , na
kuwashangaa wanaoendesha humuma hizo kwani haziwezi kusaidia kutatua
changamoto za kisiasa .
“Ni jambo la akushangaza kuona
mikarafuu , minazi pamoja na mihogo inafanyiwa hujuma namna hii , ni
vyema vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili wausika
wapatikane na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ”alisisitiza.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
Mwanajuma Majid Abdalla akizungumza katika eneo la tukio alisema
Serikali imejapanga vyema kukabiliana na vitendo vya hujuma na kuwataka
wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi kufanikisha kukamatwa kwa
wahusika wa vitendo hivyo .
Alisema kwamba Serikali
inategemea zao la Karafuu pamoja na minazi kwa ajili ya kukuza uchumi
wake , na kwamba kitendo cha kukatwa kwa mikarafuu sio tu kwamba
kinarudisha nyumba maendeleo ya mwananchi bali pia na Taifa kwa ujumla .
“Matendo haya kwa kweli sio
kama yanaathari kwa mwenye shamba pekee , bali hta uchumi wa Nchi
unaathirika kwani Serikali inategemea sana zao la karafuu kupata fedha
za kigeni ”alieleza .
Kwa upande wake kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan ameahidi kwamba
askari wataendesha doria na msako wa kuwasaka wahusika ili waweze
kufikishwa kwenye mahakamani .
Alisema kwamba katika msako huo
, watawatumia askari Shehia , Polisi jamii pamoja na wananchi wa
kawaida na kuongeza kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua hata kama
watakuwa nchi ya Mkoa huo .
Kwa hili hatutakuwa na huruma
na mtu , tutafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za jeshi ,pia
tutawatumia askari shehia , polisi jamii pamoja na raia wema abao
wamekuwa wakitupa taarifa ”alisisitiza .
Hivyo Kamanda shekhan amewataka
wananchi kutotumia fursa hiyo kutoa taarifa ambazo sio sahihi na ambazo
zinawahusu wananchi wenye chuki binafsi. Na kwamba jeshi la polisi
litazifanyia uchunguzi taarifa hizo kabla ya kuzichukulia hatua .
Matendo ya hujuma kwa baadhi ya
mali za wananchi yanaendelea kutokea katika mikoa ya Pemba baada ya
kumalizika uchaguzi Mkuu wa marejeo uliofanyika machi 20 mwaka 2016
yakihusishwa na itikadi za kisiasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni