Omar Khamis Othman amewataka wakulima wa karafuu na wadau kulilinda zao hilo
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba Omar Khamis Othman amewataka wakulima wa karafuu pamoja na wadau
wengine wa karafuu kuchukua juhudi za makusudi kulilinda zao hilo ili
liendelea kuleta tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla .
Amesema kwamba kila mdau wa
karafuu analo jukumu la kuhakikisha anaulinda mkarafuu dhidi ya vitendo
vya hujuma kwa kuhakikisha zao hilo linabaki salama na mkulima
ananufaika .
Akifunga mkutano wa wadau wa
karafuu uliofanyika kwenye ukumbi za zamani wa chuo cha uwalimu
benjemini mkapa Wete Mkuu hu wa Mkoa amesema kwamba vitendo vya kukatwa
mikarafuu ovyo kwa ajili ya shughuli za kijamii unapaswa kukomeshwa .
Ameeleza kuwa kila suala la
kuulinda mkrafuu dhidi ya vitendo vya hujuma si kazi ya serikali wala
taasisi zake , na kuongeza hilo ni jukumu la kila mmoja bila ya kujali
nafasi yake wala cheyo chake kwani karafuu unafaida kwa jamii yote .
“Hili ni zao kuu na tegemeo la
maendeleo ya uchumi wan chi , hivyo kila mmoja wetu analo jukumu la
kuhakikisha kwamba anachukua hatua za kuulinda mkarafuu pamoja na
karafuu dhidi ya matendo ya hujuma ”alifahamisha.
Mapema Mkurugenzi wa Mfuko wa
maendeleo ya karafuu Ali Suleiman amesisitiza uwamuzi wa Shirika
kutowalipa fidia watoto waliochini ya umri wa miaka 18 wanaopata ajaliw
akati akichuma karafuu ..
Amesema kwa mujibu sheria za
kimataifa ni kosa la jinai kumtumikisha mtoto aliye chini ya umri wa
miaka 18, na uwamuzi wa Shirika pamoja na mfuko umelenga katika kumlinda
mtoto dhidi ya vitendo vya utumikishwaji .
“Kwa msimu huu Shirika
halitakuwa tayari kumlipa fidia mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18,
baada ya kuanguka kwenye mkarafuu wakati akichuma karafuu , hivyo
tunawaomba sana wamiliki wa mashamba ya jarafuu hakikisheni kwamba
watoto hawapati nafasi ya kuchuma karafuu ”alisisitiza .
Nao baadhi ya wakulima
waliliomba Shirika kuwachukulia hatua za kisheria wakulima ambao
wameshindwa kurejesha mikopo , kwani wamekiuka masharti ya mikataba yao .
Walisema kuendelea
kuwabembeleza wakulima hao wakati wamekiuka mikataba hiyo ni kusababisha
shirika kushindwa kuwakopesha wakulima wengine kwani fedha hizo bado
ziko mikononi mwa wachache .
Mkutano huo uliwashirikisha
wadau wa karafuu wakiwemo wakulima , masheha , madiwani , watendaji
kutoka Serikalini Kuu ambapo pia umetumika kutoa zawadi kwa wakulima
bora .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni