SERIKALI: MFUMO WA MALIPO YA UZEENI UPO MBIONI KUANZA
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akifuatilia neno la ukaribisho alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa
Mtandao wa Asasi zinazojishughulisha na Wazee Tanzania katika ukumbi wa
Maktaba Kuu ya mkoa wa Dodoma juzi.
Baadhi ya wazee wa Mkoa wa Dodoma wakijitambulisha kwa Waziri wakati wa Mkutano huo.
Msoma risala ya wazee wote wa Tanzania Bi Clotrida Kokupima kutoka wilaya Kasulu Mkoani Kigoma akisoma risala hiyo.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa
hotuba yake alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Asasi
zinazojishughulisha na Wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya
mkoa wa Dodoma juzi.
Wazee wakifuatilia hotuba ya Waziri
Baadhi ya wazee wakiwa katika mkutano huo.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta
jambo na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Dkt. Tom Mtoi mara baada ya
kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Asasi zinazojishughulisha
na Wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya mkoa wa Dodoma juzi.
……………………………………………………………………………………………..
Ramadhani Juma, OFISI YA MKURUGENZI DODOMA
SERIKALI imesema mchakato wa
kuwaingiza wazee wote wasio katika ajira rasmi hapa nchini kwenye mfumo
wa malipo ya uzeeni uko katika hatua za mwisho na kwamba wakati wowote
kundi hilo litaanza kunufaika na mpango huo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati
akizungumza na wazee mkoani Dododma alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa
asasi zinazojishughulisha na wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba
Kuu ya Mkoa wa Dodoma juzi.
Alisema wazee wasio katika ajira
rasmi wamefanya mambo makubwa katika maendeleo ya nchi kwa muda mrefu
sasa hivyo sio sahihi kuachwa nje mfumo wa pensheni ya uzeeni na kwamba
sasa ni wakati muafaka kutambua uwepo wao na mchango mkubwa katika
uchumi wa Taifa.
Amebainisha kuwa, Serikali ya
awamu ya tano chini ya Mh. Rais Dkt. John Magufuli haitashindwa
kuwahudumia wazee wa nchi hii ambao idadi yao kwa sasa inakadiriwa kuwa
milioni 2.5 na kwamba hilo ni kundi kubwa ambalo halipaswi kutengwa.
Waziri Ummy Mwalimu pia ametoa
agizo kwa Halmashauri zote nchini kutenga vyumba maalum kwa ajili ya
kuwapatia huduma za afya wazee na kuondokana na dhana ya ‘dirisha la
wazee’ huku akiimwagia sifa Halmashauri ya Wilaya Magu Mkoani Mwanza kwa
kuonesha mfano huo na kwamba wilaya nyingine ziige hatua hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri huyo
ametoa wito kwa taasisi za fedha nchini kuwaamini na kutoa mikopo kwa
wazee badala ya kuwaona kama kundi lisiloweza kuzalisha kwani mzee
anaweza kufanya shughuli za kuichumi hata akiwa na umri wa miaka 75 hadi
80.
“Wazee wengi wameendelea na
shughuli za kuzalisha mali hadi wanafikia umri wa 75 hadi 80 hivyo
mabenki yasiwatenge wazee katika kuwawezesha kimitaji ili waendelee na
uzalishaji” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni