Bodi ya PBPA yazinduliwa rasmi.
By Newsroom on June 10, 2016
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Nishati,Dkt. Mhandisi
Juliana Pallangyo wapili kushoto, akimkabidhi vitendea kazi, Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) Dkt. Steve
Mdachi( wa pili kulia) wanao shuhudia ni mjumbe wa bodi hiyo Salum
Mnuna( kulia) na Mkurugenzi wa PBPA Michael Mjinja( kulia)
Wajumbe
wa Bodi ya PBPA pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na
Madini wakiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( katikati) mara
baada ya kuzindua rasmi bodi hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa PBPA wakifuatilia uzinduzi wa bodi yao katika ukumbi
wa mikutano wa Wakala huyo jijini Dar es salaam hivi karibuni.
…………………………………………………………………………………………………..
Na Zuena Msuya, Dar es salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo amezindua Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja
nchini (PBPA).
Akizungumza mara baada ya
kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es salaam, Dkt Pallangyo alisema kuwa PBPA
inapaswa kufanya kazi kama ilivyoelekezwa ili kuleta ufanisi kwa taifa.
Alisema kuwa Bodi hiyo imeaminiwa
na ndiyo maana imepewa dhamana ya kusimamia Wakala wa Uagizaji wa
Mafuta kwa pamoja nchini, hivyo ni vyema kuthibitisha uaminifu huo kwa
kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.
Wakala huo ulianzishwa rasmi
mwaka 2015 kwa lengo la kusimamia usalama wa mafuta ya Petroli, Diseli,
Mafuta ya ndege JET na Mafuta ya taa; Pia, kuhakikisha uwepo wa mafuta
nchini wakati wote na kuhakikisha kuwa wale wote walioagiza mafuta
wanapata malipo stahiki na kwa wakati.
Aidha Dkt Pallangyo alisema kuwa
bodi hiyo inapaswa kumshauri Waziri wa Nishati na Madini juu ya muundo
mzima la uagizaji mafuta kwa pamoja ili kuongeza ufanisi wa huduma hiyo.
Majukumu menhine ni kusimamia mapato na matumizi ya wakala huyo, ajira, usalama kazini na miongozo yote inayohusu PBPA.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Bodi husika Dkt. Steve Mdachi aliahidi kuwa hawataingusha Serikali na
pia watatimiza kile kilichokusudiwa ili kuleta tija na ufanisi kwa
taifa.
Dkt. Mdachi alisema kuwa kazi yao
ya kwanza ni kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa PBPA wanakuwa katika
mazingira mazuri na bora ya kazi ili waweze kutimiza majukumu yao kwa
viwango vinavyotakiwa.
Bodi ya PBPA imeteuliwa na Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo hivi karibuni na
itaongozwa na wajumbe watano akiwemo Mwenyekiti pamoja na wajumbe wanne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni