Serikali kushirikiana na kampuni ya TING kuboresha mapato ya Uwanja wa Taifa.
Kaimu
 Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza
 na wawakilishi kutoka Kampuni ya TING(hawapo pichani) kuhusu 
kushirikiana na Serikali kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia 
matangazo.
Afisa
 Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos akifafnua jambo 
katika kikao kati ya kampuni yake na Serikali kilicholenga kushirikiana 
katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Mkuu
 wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah akionesha jinsi kampuni yake 
itakavyoweka miundombinu ya kuweka matangazo ndani ya uwanja wa taifa 
katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika 
kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Baadhi
 ya maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifatilia 
kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha
 mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
…………………………………………………………………………………………………………….
(Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM)
Serikali imeanza majadiliano na kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo uwanjani hapo.
Akizungumza hapo jana wakati wa 
kikao kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kampuni 
hiyo, Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge
 amesema kuwa Serikali imefarijika kupata maombi hayo kutoka kampuni ya 
TING ya kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo ambayo 
yatawekwa katika maeneo ya uwanja huo.
“Ndugu zetu TING wamekuja na wazo
 zuri sana na tumelipokea na tunaahidi kuliangalia kwa jicho la tatu 
kwani ni fursa ya pekee kwetu, sio kuboresha mapato tu bali kutangaza 
uwanja wetu na kuendeleza michezo kwa ujumla” alisema Bw. Nkenyenge.
Aliongeza kuwa ni wakati sasa wa 
Serikali pamoja na Wananchi kufaidika na uwanja wao ambao ni wa kipekee 
katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwani fursa hiyo itasaidia pia
 kuendeleza Kijiji cha Michezo Changamani ambao pia ni mpango wa 
Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji 
Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos amesema kuwa kampuni yake 
itatoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Wizara na ni azma yao kuona 
wananchi wanaona faida ya kuwa na uwanja wa kisasa ambao utawaletea 
mafanikio katika maendeleo ya michezo nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa 
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na 
Michezo Bi. Esther Yonael ameipongeza kampuni ya TING kwa kuona fursa na
 kuitumia kwani kuna kampuni nyingi zinaweza kuwa ziliona hiyo fursa hii
 lakini sikakosa uthubutu wa kuleta maombi Wizarani kushirikiana katika 
suala hilo ambalo linafaida kwa pande zote mbili.
Aidha, Mkuu wa Masoko kutoka TING
 Bi. Bernice Hannah ameihakikishia Serikali kuwa wamejipanga vizuri na 
wamefanya utafiti wa kina wa mradi huo na kuona kuwa unawezeka 
ukafanyika na kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo nchini.
Kampuni ya TING imedhamiria 
kushirikiana na Serikali katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa na 
imejipanga kuwekeza Shilingi Billioni moja kwa miaka minne katika 
miundombinu na wataalam.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni