  | 
| mbunge  wa Singida 
Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu (kulia) akimpokea  waziri wa Kilimo ,Mifugo 
na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya  kikazi wilaya ya 
Manyoni jana | 
  | 
| Waziri Nchemba  akisalimiana na mbunge Nyalandu (kulia) | 
  | 
| Waziri 
 wa  kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akiwa ameongozana na 
viongozi mbali mbali  kuingia  ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima 
wa Tumbaku Manyoni  | 
  | 
| Mbunge
 Lazaro  Nyalandu kulia akiwa na waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw 
Mwigulu Nchemba wakati akisaini kitabu cha  wageni  ofisi ya mkuu wa 
wilaya ya Manyoni mkoani Singida  | 
  | 
| Waziri Nchemba  akiingia ukumbi wa mkutano kati yake na  wakulima wa Tumbaku manyoni  | 
  | 
| Wakulima wa Tumbaku  wakisalimiana na waziri Nchemba   | 
  | 
| Baadhi ya madiwani  wakulima wa Tumbaku manyoni wakimpokea  waziri Mwigulu Nchemba  | 
  | 
| Baadhi ya  wakulima wa Tumbaku  wakiwa  ukumbi wa mkutano kati yao na waziri Nchemba  | 
  | 
| Mbunge
 wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu  akitambulisha  viongozi mbali 
mbali kabla ya  mkutano wa  wakulima wa Tumbaku kuanza  | 
  | 
| Waziri
 wa  Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akizungumza na  
wakulima wa Tumbaku wilaya ya manyoni mkoa wa Singida jana | 
  | 
| Diwani 
 wa kata ya Mitundu wilaya ya Manyoni Bw Andrea Madole  akimkabidhi 
nyalaka mbali mbali za uthibitisho wa michango kandamizi  
wanayobambikizwa  wakulima wa Tumbaku na Kitengo  cha AMIS   waziri wa  
kilimo ,mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae alitangaza   kufuta 
michango  hiyo  | 
  | 
| Wakulima wa Tumbaku  wakitoa kero  zao kwa  waziri Nchemba (hayupo pichani) | 
  | 
| Wabunge  wakisikiliza kero  za  wakulima wa Tumbaku  | 
Waziri wa Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu 
Nchemba  (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Singida Kaskazin Bw
 Lazaro Nyalandu  wakati  akieleza kilio  cha wakulima wa Tumbaku  
wilaya ya Manyoni wakati wa  mkutano wa  waziri Nchemba na wakulima wa 
Tumbaku  uliofanyika  ukumbi wa CCM Manyoni jana
…………………………………………………………………………………………….
Na MatukiodaimaBlog,Manyoni
WAZIRI wa  kilimo ,mifugo na  uvuvi  Bw Mwigulu  Nchemba amefuta 
michango  hewa iliyokuwa ikichangiwa na wakulima wa Tumbaku  kwa  UNION 
kwa  kupitia  kitengo  cha AMIS huku akiagiza serikali  ya  wilaya ya 
Manyoni  kuwachukulia hatua  kali aofisa  ushirika mkoa  Andru Msafiri 
na afisa  ushirika Wilaya   hiyo Bw Alfred Sekiete iwapo watabainika  
kuhusika  deni la bilioni  7  ambalo wanadaiwa benki wakulima  wa 
tumbaku.
 
Waziri Nchemba  alilazimika kutoa maagizo  hayo  baada  ya  
wakulima  wa zao hilo la Tumbaku  kulalamikia utaratibu mbaya wa baadhi 
ya  viongozi wa UNION na APEX pamoja na baadhi ya maofisa  ushirika   
kujinufaisha  kupitia mgongo  wa  wakulima hao.
 
Akitoa agizo  hilo  jana mjini Manyoni  wakati wa  
mkutano  wa  pamoja kati yake na  wakulima wa  Tumbaku na viongozi  
mbali mbali  wa Serikali  ya  wilaya ya Manyoni na wabunge  wanaotoka  
wilaya ya Maeneo  yanayolimwa Tumbaku  mkoani Singida.
 
Waziri Nchemba  alisema  kuwa  baadhi  ya mambo  ambayo 
serikali  ya Rais Dr John Magufuli  haipendi  kuona ni  pamoja na  
wakulima kubebeshwa mizigo mikubwa ambayo kimsingi haiwasaidii kupiga 
hatua kimaendeleo  zaidi ya  kuwatesa .
 
Alisema  inashangaza  kuona   wakulima  hao  kuendelea  kuumizwa
 na  viongozi  wachache ambao  wamegeuza  wakulima ni  kichaka cha  wao 
 kujificha  kujinufaisha  kupitia wakulima.
 
“ Mambo  ya ajabu  sana  hiki kitu  kinaitwa AMIS ni kuwatoza  
wakulima michango ya ajabu ajabu  eti  wakulima  kutozwa  dola 1200 kwa 
 ajili  ya kusafirisha Tumbaku toka  Dar es Salaam kwenda UNION   pia  
wanachangia dola 10 kwa  kutunza  kumbukumbu zao  ,dola 3 kupakia na  
kushusha mara mchango kwa ajili ya ADMIN   mambo ya ajabu kabisa 
wakulima wanahusika  vipi na malipo maadmin yani wanatumia lugha  za  
kijanja kijanja  kuwaibia  wakulima ADMIN wa makundi kama yale ya 
Whatsap kwa wakulima  tena…sasa kuanzia leo natangaza  kufuta michango  
hii isiyo na maelezo ya kutosha na kuagiza  kujipanga upya kwa  
kuwashirikisha   wakulima na taarifa  hiyo ndani ya siku 7 niipate “
 
Waziri chemba  alisema  kuwa kabla ya  kuanza  kuwatoza  
wakulima hao michango ni  vizuri  makubaliano ya  michango  hiyo 
yafanyike  upya kwa kuwashirikisha  wakulima na sio kuendelea  kutumia 
taratibu  za  zamani ambazo ni mzigo kwa  mkulima.
 
Kuhusu maafisa  ushiriki  kudaiwa  kukopa  benki  kupitia mgongo
 wa  wakulima  wa  tumbaku na  kupelekea  wakulima hao  kudaiwa  deni  
benki  la Tsh bilioni 7 aliagiza mkuu wa  wilaya ya Manyoni kuagiza 
wakaguzi  na wataalam wake  kufanya  uchunguzi  na iwapo itabainika  
kuwa maofisa  hao  walihusika na deni  hilo  hatua  stahiki  kuchukuliwa
 dhidi 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni