Jumapili, 12 Juni 2016

Nuh Mziwanda ft Ali Kiba Jike Shupa Official Video


Nuh Mziwanda ameelezea jinsi uhusiano wake na Shilole ulivyokuwa kwa dakika 3:50!
Nuh 1
Kwa video ya wimbo wake Jike Shupa aliomshirikisha Alikiba, Nuh ameuelezea uhusiano huo ulitawaliwa na mateso, wivu uliokithiri, kichapo na tabu za kila aina.
Nuh 2
Kuthibitisha kuwa wimbo huo unamlenga ex wake, amemtumia msichana anayefanana copyright na Shilole. Kwenye video hiyo pia Nuh hakuacha kuonesha tattoo ambazo Shilole alizichora enzi wakiwa wakiwa wapenzi.
shishi Kushoto ni Shilole real. Kulia ni video queen kwenye Jike Shupa
Nuh amemuonesha msichana huyo kama mjeuri na ambaye wakati mwingine anarudi nyumbani akiwa chakari. Ni video nzuri, icheck hapo chini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni