Jumatano, 15 Juni 2016

MABONDIA GALILE NA MAPAMBANO KUMALIZA UBISHI JULAI 24 MUSOMA BAR


Mdau wa masumbwi nchini Jumanne Mbwembwe akiwainua mikono juu mabondia Imani Mapambano kushoto na Seleman Galile kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa julai  24 katika ukumbi wa Musoma Bar Tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Iani Mapambano kushoto na Selemani Galile wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa julai 24 katika ukumbi wa Musoma Bar tasndika Picha na SUPER D BOXING NEWS
 
Mabondia Imani Mapambano kushoto akitunishiana misuli na Selemani Galile baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga julai 24 katika ukumbi wa Musoma Bar tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS.
………………………………………………………………………………………………………
 
Na Mwandishi Wetu
 
MABONDIA Imani Mapambano na Selemani Galile wamesaini mkataba wa kuzipiga Julai 24 katika ukumbi wa Musoma Bar uliopo Tandika Dar es salaam
 
Akizungumza baada ya kusainishwa kwa mabondia hao mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’
amesema kuasini mkataba kwa mabondia hao  baada ya kutambiana mara kwa mara utaonyesha nani ni mbabe kati yao watakapopanda ulingoni Julai 24 mwaka huu, nimeamua wapambane julai 24 katika ukumbi wa Musoma Bar ili kumaliza ubisha wao.
Mpambano huo utakuwa wa ubingwa wa Taifa utakaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah ‘Ustaadhi’
Aliongeza kwa kusema kuwa mipambano mingine ya utangulizi itatangazwa kadri watakavyo ingia mikataba na mabondia mbali mbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni