Jumapili, 31 Julai 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MKUTANO TINDE, ISAKA NA KAHAMA MKOANI SHINYANGA

M1Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea Nzega mkoa Tabora.
M2Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza jukwaani wimbo wa kwaya ya Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga kabla ya Kuhutubia mamia ya wakazi Kahama mkoani Shinyanga.
M4Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli mara baada ya kuwasalimia wananchi waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais katika viwanja hivyo vya Kahama.
M5Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Isaka mkoani Shinyanga.
M7Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa Chadema mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani Shinyanga.
M8Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na Wanakwaya wa Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano Kahama mjini mkoani Shinyanga.
M9Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuoneshwa picha na kijana mmoja aliyeishika picha hiyo.
M10Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Tinde mkoani Sinyanga.
PICHA NA IKULU

SERIKALI KURASIMISHA MAKAZI HOLELA JIJINI DAR ES SALAAM.

O1Diwani Kata ya Kimara Mhe. Pascal Manota akihamasisha wananchi wa Mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara kushirikiana na Wataalam wa masuala ya Ardhi ili kuruhu upimaji wa maeneo yao walipofanya mkutano wa uhamasishaji juu ya Urasimishaji wa Makazi holela.
O2Kaimu Mkurugenzi Urasimishaji Makazi holela Bi. Bertha Mlonda akielezea faida za urasimishaji katika mkutano wa Uhamasishaji kwa wanachi wa Kata ya kimara mtaa wa Mavurunza.
O3Badhi ya wakazi wa Mtaa wa Mavurunza waliohudhuria mkutano wa Uhamasishaji kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela, wakiwasikiliza viongozi wa Serikali za Mitaa (Hawako pichani) pamoja na wataalam kutoka Sekta ya Ardhi walipokuwa wakitoa elimu kwa wakazi hao.
O4Hamza Khatibu, Mkazi wa Mtaa wa Mavurunza akiuliza swali kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na wataalam wa Sekta ya Ardhi walipokuwa katika mkutano kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela.
O5Alama inayotenganisha kiwanja kimoja na kingine inayowekwa na wataalam wa upimaji kutoka Wizara ya Ardhi, wakishirikia na wataalam kutoka Manispaa ya Kinondoni.
O6 O7 O8Wataalam kutoka Wizara ya Ardhi na Manispaa ya Kinondoni wakiandaa ramani za maeneo ambayo tayari yamefikiwa kwa ajili ya kupimwa na kurasimisha makazi holela katika Kata ya Kimara, Mtaa wa Kilungule B.
……………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeanza kupima viwanja zaidi ya 25,000 kwa wakazi wa kata za Kimara na Saranga zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kurasimisha makazi holela.
Akizungumza kwa nyakati tofauti Kaimu mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela Bi. Bertha Mlonda amesema, Uendelezaji Miji ni kwa mujibu wa Sheria ya MipangoMiji na una faida nyingi kwa wanachi. Alisisitiza kwamba, Maendeleo ya sehemu yeyote hutokana na miundombinu ya sehemu husika pamoja na huduma za kijamii zinazopatika.
Mlonda amewaasa wananchi haswa wa Kata za Kimara na Saranga kutoa ushirikiano kwa wataalam ambao wameanza kupima maeneo yao ili kuondokana na tatizo la Makazi Holela kwa wakazi hao kwani upimaji huo utabadilisha taswira na hadhi ya maeneo yao.
Kwa sasa Urasimishaji umeanzia katika Kata za Kimara na Saranga, baada ya hapo yatafuata maeneo yote yenye sifa za urasimishaji katika jiji la Dar es Salaam, na mikoa yote ya Tanzania. Zoezi hili litakuwa likitekelezwa kwa awamu kulingana na maeneo yatakavyobainishwa.

MKWASA AAHIRISHA KAMBI TAIFA STARS

mkwasaserenaKutokana na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu, imefahamika.
Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC.
Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki wa klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.
Taifa Stars ina mchezo na jijini Lagos, Nigeria Septemba 2, 2016 ambao ni wa kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad kujitoa. Wachezaji ambao Mkwasa aliwaita mapema wiki hii ni:
Makipa:
Deogratius Munishi
Aishi Manula
Benny Kakolanya
Mebeki:
Kelvin Yondani
Aggrey Morris
Oscar Joshua
Mohamed Husein ‘Tshabalala’
Juma Abdul
Erasto Nyoni
Viungo:
Himid Mao
Mohamed Ibrahim
Shiza Kichuya
Jonas Mkude
Ibrahim Jeba
Mwinyi Kazimoto
Farid Mussa
Juma Mahadhi
Hassan Kabunda
Washambuliaji:
Simon Msuva
Joseph Mahundi
Jamal Mnyate
Ibrahim Ajib
John Bocco
Jeremia Juma

MAKOCHA TANZANIA WAANZA KUIVA

lesencMakocha 20 wa Tanzania wanaofanya kozi ya Leseni A kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wamemaliza kozi hiyo hatua ya kwanza na kusema, “Tumenolewa na sasa tumeiva vya kutosha,” amesema mmoja wa wanafunzi hao, Wilfred Kidao leo saa Julai 30, 2016 wakati Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Kidao amesema japo kozi hiyo ilikuwa hatua ya kwanza ‘Module 1’ kwa sasa wameiva kiasi kwamba watakapomaliza Novemba, mwaka huu wana uhakika wa kupeleka vyeti vyao sehemu yoyote duniani kuomba kazi na kushinda kwa kuwa wameiva vilivyo. Wakufunzi wa kozi hiyo walitokea CAF, Sunday Kayuni na Salum Madadi ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.
Baada ya kusikiliza kauli hiyo ya Kidao, Rais wa TFF Jamal Malinzi moja kwa moja akawasisitiza makocha hao kufanya kazi kwa juhudi na kuwaeleza kuwa hatua waliyofikia ni kubwa kwa kuwa baadhi ya makocha kutoka nje hawana vyeti na kukosa sifa ya kufundisha timu kubwa ikiwamo timu za mataifa ngazi mbalimbali.
Rais Malinzi alitaka makocha hao kuangazia mpira wa miguu kwa wavulana wengi wakiwa wanatokea katika mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel pamoja na soko la wasichana ambalo kwa sasa linashika chati kila kona ya dunia.  
Naye, Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia alimpongeza Rais Malinzi kwa namna anavyoratibu na kuzikubali kozi mbalimbali za waamuzi na makocha. “Kwa muda mrefu au tuseme kwa miaka mingi hakujafanyika kozi nyingi kama kipindi cha uongozi wako ukisaidiana na mimi pamoja na kamati nzima ya utendaji pamoja na sekretarieti.”
“Fanyeni utafiti ninyi makocha. Utaona kuwa sehemu kubwa nchi za Afrika zimefanikiwa kwa kutumia makocha wazawa. Leo ninyi ni makocha wa ngazi ya juu kabisa hivyo mna uwezo wa kufanya vema na kusaidia timu zetu na timu za taifa,” alisisitiza Karia.

SINAI MISSIONS INTERNATIONAL (SMI) YAFANYA MKUTANO WAKE MKUU WA MWAKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

????????????????????????????????????Mgeni rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Bishop Dr Kameta (katikati) akizungumza na wanachama wa Shirika la kidini linalotoa huduma kwa makanisa na mashirika yanayofanya kazi ya kueneza injili ulimwenguni lijulikanalo kama  SINAI MISSIONS INTERNATIONAL(SMI) wakati wa mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika jijini Dar es Salaam Lengo  la mkutano huo ilikuwa ni kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI. kulia  ni Rais wa shirika hilo Ing.Bishop Piter M.Sanga.na kushoto Katibu Mkuu anaemaliza muda wake Bishop Pite W.Chinyama kutoka Zambia.na Mweka Hazina anayemaliza muda wake Msh Raphael Muhagama kutoka Tanzania.
????????????????????????????????????Wajumbe wa Mkutano.
????????????????????????????????????Mkutano ukiendelea.
????????????????????????????????????????????????????????????????????????Wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wakifuatilia mada mbalimbali.
????????????????????????????????????Viongozi wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio wakati wa mkutano mkuu wa mwaka kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.
????????????????????????????????????Wajumbe wa mkutano wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio.
????????????????????????????????????Wajumbe wa mkutano mkuu wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio wakati wa mkutano mkuu wa mwaka kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.
????????????????????????????????????Mgeni Rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Bishop Dr Kameta (kushoto), pamoja na Mtafisiri ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirika la MSI, Bishop Gilibert Biyengo.wakihutubia Mkutano Mkuu wa Mwaka.
????????????????????????????????????Mgeni rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekosite, Bishop Dr Kameta (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa SINAI MISSIONS INTERNATIONAL(SMI) uliofanyika jijini Dar es Salaam kwaajili ya kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG

JPM AKOSHWA NA DC WA IGUNGA JOHN MWAIPOPO, AAMURU STENDI YA BASI NA SOKO VIANZE KAZI JUMATATU

 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani ambako nako pia wana sehemu za Biashara.
  Rais  Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo wakati akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
  Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt. Magufuli kuhusiana na  Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. Rais ameitaka SUMATRA ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi Jumatatu. Pia ameiagiza halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu za biashara bila kuzitumia katika soko jipya wathibitiwe mara moja.
 Wananchi wa Igunga wanalipuka kwa furaha na Mzee huyu anatoa  noti ya shilingi 10,000/- akitaka kumtuza  Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua changamoto za Stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
Rais Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele wa grade One kutoka uongozi wa wilaya ya Igunga  wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
PICHA NA IKULU

Wadau wa Sanaa nchini wahamasishwa kudhamini na kufadhili Mashindano ya Urembo bila ubaguzi.

S1Miss Dar Indian Ocean aliyemaliza muda wake, Camilla John (katikati) akimvisha skafu Mshindi wa Mashindano ya Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo (kushoto) mara baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
S2Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na warembo wenzie ambaye ni Mshindi wa pili na wa tatu mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
S3Kaimu Mkuregenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Francis Songoro (kulia) akimpongeza Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
S4Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………..
Na. Benedict Liwenga-WHUSM.
Wadau wanaojishughulisha na masuala ya Sanaa nchini wamehamishwa kujitokeza kwa wingi katika kusaidia maendeleo ya Sanaa kwa kudhamini na kufadhili mashindano ya urembo bila kubagua.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Francis Songoro wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Anastazia Wambura ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Miss Tanzania Indian Ocean 2016 yaliyofanyika katika Ukumbi wa MRC uliopo Mikocheni jijini hapa.
Akiwasilisha hotuba hiyo, Songoro amesema kwamba kazi inayofanywa na wadau wa sanaa ni hatua ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni ambayo inasisitiza jamii na wakuzaji sanaa kuendeleza ubunifu katika kazi za kiutamaduni.
Ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara yake inathamini na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau hao hasa katika kukuza na kuviendeleza vipaji vya vijana nchini, hivyo amewapongeza wadau hao kwa moyo wao wa kujitoa na kuwataka kuendeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 katika Sura ya 9 kifungu cha 9:5:8 ambacho kinasisitiza na kuhimiza watu binafsi pamoja na Mashirika kuwekeza rasilimali katika sekta ya utamaduni.
‘’Maonyesho haya ni ishara tosha kuwa sanaa ni kazi, ajira, biashara na burudani, hivyo kipekee nawapongeza sana’’, alisema Songoro.
Aliongeza kuwa, Warembo ambao wameshiriki katika mashindano hayo wanautangaza utalii wa ndani na nje ya nchi na kwa kufanya hivyo wanaiwakilisha vyema Tanzania Duniani katika mashindano ya Miss World na pia kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, amewataka warembo ambao hawakubahatika kuibuka washindi katika mashindano hayo kutokata tamaa, bali waitumie fursa hiyo hususani ya elimu waliyoipata wakiwa kambini kwa kuisadia jamii inayowazunguka na kuwa wanawake wa mfano wa kuigwa katika kujitambua na kujiamini.
‘’Mtambue kwamba, siyo wote mtakaoibuka washindi na kuendelea mbele katika mashindano haya, niwaombe wale ambao hamtashinda msivunjike moyo, bali mkaitumie elimu mliyoipata na yale ambayo mmejifunza mkiwa kambini kwa kuisaidia jamii inayowazunguka na muwe wanawake wa mfano wa kuigwa’’, alisema Songoro.
Katika mashindano hayo, Mshindi wa Kwanza aliyeibuka na kunyakua taji hilo ni Jackline Kimambo ambaye alipatikana kati ya tano bora  na kuvikwa taji la Miss Tanzania Indian Ocean 2016 na Mshindi wa pili ni Regina Ndimbo huku wengine waliobaki kwenye tano bora wamepata fursa ya kuingia katika mashindano ya Miss Kinondoni.
Shindano hilo lilihusisha jumla ya washiriki wapatao 20 ambapo mmoja kati yao ndiyo aliyeibuka mshindi na lilidhaminiwa na wadau mbalimbali wakiwemo Mikocheni Resort Centre, Mlimani TV, Channel Ten, Darling, Helmic, Tanzania Breast Cancer Foundation, Magic FM, Jozi Lounge, Kiss Printers pamoja na NTS.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NZEGA MKOANI TABORA.

J1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Mkoani Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka  mara baada ya Kuwasili Nzega mkoani Tabora jana kwa ajili ya ziara ya kikazi.
J2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Tabora Al-Haji Ramadhani Rashid katika viwanja vya  Stendi ya Nzega kabla ya kuhutubia mamia ya wakazi wa Nzega.
J3 J4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  mamia ya wananchi katika viwanja vya Stendi ya Nzega wa mkoani Tabora jana.
PICHA NA IKULU

NAIBU WAZIRI MPINA AZITAKA RADIO ZA JAMII KUHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA

hag1Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (katikati) akiangalia samaki katika soko ya wilaya ya Masasi akiwa katika ziara yake ya usafi na ukaguzi wa mazingira mjini Masasi, (kilia) ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bw. Selemani Mzee.
hag2Aliyeinama katikati akikusanya uchafu ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira Wilayani Masasi mwishoni mwa wiki.
hag4Bw. Benjamini Elias (kulia) Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Masasi akitoa taarifa na maelezo ya hali ya usafi  wa soko la mji wa Masasi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina (kushoto), wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira  mjini Masasi. (PICHA NA EVELYN MKOKOI)
……………………………………………………………………………………………
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amezitaka Radio za jamii kuhamasisha usafiri wa mazingira nchini. Naibu  Waziri Mpina ametoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki siku ya usafi kitaifa,  mwishoni mwa wiki wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Akitolea Mfano wa Radio Pride FM ya Mjini Mtwara yenye kupatikana katika frequencies 87.8 mjini Mtwara, ambayo imeanzisha kampeni ya usafi katika mkoa wa mtwara na wilaya zake kwa kufanya vipindi vya moja kwa moja na kutembelea wilaya za mkoa huo kufanya usafi wa mazingira kwa vitendo.
Kwa Upande wake Bw. JUma Andrea Manager uzalishaji wa kituo hicho cha Radio, alisema kuwa lengo kubwa la kituo hicho kuhamasiha usafi ni kuunga mkono agizo la Mhe. Rais kwa kuwaweka pamoja wananchi, kuweka muamko na hamasa ili kujenga tabia ya kupenda usafi na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa homa ya matumbo na kipindipindu.
Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara katika majumuisho ya ziara yake Wilayani Masasi, Naibu Waziri Mpina aliwataka viongozi wa mkoa huo kuunda sheria ndogondogo za mazingira zitakazo watoza faini wananchi waharibifu wa mazingira mkoani humo, na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na hali ya wananchi ili waweze kujifunza na kujijengea tabia ya usafi.
“Nimeona kuwa uchomaji moto misitu ovyo hapa kwenu umekithiri, uchomaji moto taka nao siyo njia nzuri ya uondoshwaji wa taka,hiyo kuwe na miondombinu rafiki kwa uondoshwaji wa taka, na kiongozi wa mkoa ambae hatakuwa tayari kushughulikia usafi wa mazingira na yeye awe tayari kushughulikiwa alisisitiza.”
Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mkoani Mtwara ni muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa viwanda na usafi wa mazingira iliyohusisha pia ukaguzi wa machinjio ya mji wa Masasi.

TBL Group family day 2016 yafana vilivyo

tbo1Mkurugenzi Rasiriamali watu wa TBL Group David Magesa (kushoto) akimkabidhi Mercy Maliwa  zawadi kwa kuibuka mshindi wa shindano la mpango wa AfyaKwanza , wakati wa wa  Siku ya wafanyakazi wa kampuni hiyo (Family Day) iliyofanyika kwenye viunga vya  hoteli ya Fun City Kigamboni jijini Dar es Salaam
tbo2Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakisafishwa   kucha za miguu pamoja na kupakwa rangi kwenye burudani za siku ya familia
tbo3Wototo wa wafanyakazi walicheza michezo mbalimbali
tbo4Watoto wakiweza kujibu maswali ya ufahamu na kujishindia zawadi
tbo5Zoezi la Afya Kwanza lilitekelezwa kwa vitendo
tbo6Baadhi ya wafanyakazi na família zao wakipata misosi
tbo7Baadhi ya wafanyakazi na família zao wakipata misosi
tbo8Wana msondo wakimwaga burudani kwa wafanyakazi wa TBL Group
tbo9Msanii maarufu wa vichekesho  Joti alikuwepo kumwaga burudani
tbo10Burudani tele za muziki zilikuwepo
tbo11 tbo12