Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Breaking news. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Breaking news. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 1 Septemba 2016

RC ARUSHA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI


1
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo(katikati)akizungumza na Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley
Hotay(kushoto)  alipomtembelea ofisini kwake 

Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley
Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho
Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya
Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia)  baada ya mazungumzo yao.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameendelea  na  ziara yake ya kujitambulisha kwa
viongozi wa dini  ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi  baada ya kuteuliwa kushika  wadhifa huo hivi karibuni.
Mh.Gambo amekutana na  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini
Kati,Mchungaji  Solomon Masangwa , Askofu wa  Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi  na Askofu  Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro.
Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira
ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.
Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph  Magufuli kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani  halmashauri zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya  mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali  zitakazowawezesha kufanya  shughuli za uzalishaji mali.
Amewataka  wawajulishe waumini wa dini zote na serikali iko tayari  kupanga utaratibu wa maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa  elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala kisiasa.
Askofu Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aidha alishauri  kutokana na idadi ya watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo  ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya
kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
Mh. Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili  watoe mawazo yao katika kuiboresha na  kuifanya itekelezeke   kwa wepesi zaidi.

Jumapili, 17 Julai 2016

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI KIGALI, RWANDA KWA AJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WA UMOJA WA AFRIKA

KIGA1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Francis Gatare alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rwanda kwa ajili ya  kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo picha na (OMR)
KIGA2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda ,Francis Gatare  mara alipowasili kwenye Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Kigali kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na SerIkali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa rais anamwakilisha Rais Dkt  John Magufuli Katika Mkutano huo ,Picha na (OMR)
KIGA3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda,Francis Gatare kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kigali, Rwanda mara baada ya Kuwasili nchini humo kwa ajili ya Kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt John Magufuli katika Mkutano huo. (Picha na OMR)

Alhamisi, 30 Juni 2016

Mlipuko wa bomu wawaua watu 18 Somalia

  • By Newsroom on June 30 2016
Mlipuko wa bomu Somalia
Habari kutoka Somalia zinasema kuwa watu 18 wameuawa baada ya bomu kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.
Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole.
Inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi lililokuwa karibu.
Mara kwa mara wapiganaji wa Al Shaabab hulenga wanajeshi wa Serikali.

Jumatano, 29 Juni 2016

Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakar asema kesi nyingi zinazofunguliwa Zanzibar hazina mashiko

a 
Na Masanja Mabula –Pemba
MWENYEKITI wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakar amesema kuwa kesi nyingi zinazofunguliwa katika mahakama za Zanzibar hazina mashiko na zilipaswa kusuluhishwa na jamii kabla ya hazijafikishwa mahakamani .
Amesema kwamba hali hiyo inasababisha kuwepo na mrundikano wa kesi  katika mahakama , kutokana na jamii kuina mahakama kama  sehemu ya kuwasilisha malalamiko hata yale yasiyo na mashiko .
Jaji Mshibe ameyabainisha hayo wakati akifungua kikao cha siku moja cha kukusanya maoni juu ya sheria ya mirathi kwa viongozi wa dini , mahakimu , walemavu pamoja na viongozi wa kisiasa Kisiwani Pemba  katika ukumbi wa Benjemini Mkapa Wete .
Amefahamsha pamoja na kuwepo kwa vyombo vya ulinziz na viongozi wa serikali za mitaa (masheha) lakini wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuzuia matendo maovu yasitokea ndani ya jamii kabla ya kuwafikisha mahakamani .
“Kwa kipindi kimekuwako na ongezeko kubwa na kesi katika mahakama za Zanzibar na ikizifuatilia utabaini kwamba hazina mashiko , ambazo zilipaswa kusuluhishwa kabla hazijafikishwa mahakamani ”alieleza.
Aidha Mshibe alizidi kufahamisha kwamba kitendo cha jamii kusuluhisha kesi badala ya kufikishwa mahakamani pia kutaokoa fedha nyingi ambazo zilikuwa zitumike kwa ajili ya kuandaa shauri hilo  .
Alieleza kwamba iwapo kila mmoja atawajibika kuzuia matukio yasitokee ndani ya jamii , kutaleta ufanisi wa utendaji wa kazi  serikalini kwani watumishi wake hususani wa mahakama watapunguziwa mzigo wa kupokea mashauri mengi kupita uwezo wa wa kufanya kazi .
“Kama kila mmoja atawajibika kuzuia kesi kufikishwa kutaongeza pia ufanisi wa kazi kwa watendaji wa mahakama zetu , ambao kwa sasa wanapokea kesi nyingi kupita uwezo wa mahakama zenyewe ”alifahamisha.
Hata hivyo akizungumzia suala la kuongezwa watendaji wa Idara ya Mahakama , Jaji Mshibe alisema suwala hilo tayari limepatiwa ufumbuzi , lakini bado changamoto ni jamii yenyewe kutokuwa tayari kufanya suluhu kwa kesi za kawaida .
Akichangia kwenye kikao hicho , Padri wa kanisa la Anglikana Pemba Massoud Emmanuel alisema kwamba , bado jamii haijawa tayari kupokea ushauri na maelekezo kutoka kwa wananchi wa kawaida hata kama utakuwa na maana au faida kwao .
Amesema kwamba viongozi wa dini wanapowajibika katika kuelimisha jamii , hushushiwa zigo wakidaiwa kwamba wamekuwa wanasiasa , jambao ambalo linawawia vigumu kuufikisha ujumbe kwa jamii inayaowzunguka .

SMZ YAAHIDI KUENDELEZA MIPANGO YA UCHUMI INAYOCHAGIZWA KIMATAIFA

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuhakikisha mipango yote ya kimaendeleo inayochagizwa na malengo endelevu ya kimataifa inatekelezwa kwa vitendo ili wananchi waweze kunufaika.
 
Imesema katika malengo ya milennia ya 2015 serikali ilifanikiwa katika baadhi ya sekta zikiwemo sekta za elimu, afya na miundo mbinu hatua zinazotakiwa kuendelea kupewa kipaumbele na wadau wa maendeleo.
 
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli katika Mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wanaojadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani humo. Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
 
Alisema licha ya kuwepo na changamoto mbali mbali za kiutendaji katika utekelezaji wa mipango hiyo ikiwemo suala la wananchi kutokuwa na uelewa mzuri wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya dunia bado mamlaka husika zinaendelea kutoa elimu hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika Mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wanaojadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar ambao umeandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Tume ya Mipango Zanzibar chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini.
 
Reli alieleza kwamba malengo na mipango mbalimbali ya maendeleo ni kuwasaidia wananchi wa Zanzibar waweze kuondokana na tatizo sugu la umaskini, magonjwa na changamoto za kiusalama.
 
“Katika MDG tumeweza kufanikiwa kwa baadhi ya malengo ikiwemo suala la elimu na afya lakini kuna mengine bado hatukuweza kufanikiwa kuyafikia na kwa sasa tunaendelea na malengo mapya ya SDG’s ambayo tunatakiwa kuyafanyia kazi ili yaende sambamba na mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.” alisema Reli.
 
Aidha alisema bado wanajadiliana ni kwa namna gani mipango ya kimataifa tutaiingiza katika sera na mipango yetu ya kimaendeleo ili wananchi waweze kunufaika na fursa hizo za kimaendeleo na kiuchumi kwa ufanisi zaidi.
 
Alisema utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s ambayo ni 17 yanatakiwa kupewa kipaumbele kwani yanagusa nyanja mbalimbali za kijamii yakiwemo maisha halisi ya wananchi wanaostahiki kunufaika na fursa na mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) Ofisi ya Zanzibar, Anna Senga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez katika mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar.
 
Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafti, Uchumi na Kijamii nchini ( ESRF), Dkt.Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho alisema, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika SDG’s ni vyema sera na mipango endelevu ya nchi husika iweke vipaumbele vya kukuza uchumi kuanzia ngazi za chini
 
Kida alieleza kwamba katika utekelezaji wa SDG’s lazima kuwepo na mpango endelevu wa ufuatiliaji kuanzia ngazi za chini hadi taifa kwa lengo la kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa kwa mujibu wa matakwa ya malengo ya kimataifa.
 
Naye Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Ofisi ya Zanzibar, Anna Senga alisema endapo malengo ya dunia yataweza kutekelezwa ipasavyo Zanzibar itaweza kupunguza changamoto mbali mbali zinazokabili sekta za kijamii na kiuchumi.
 
Alisema UN itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika utekelezaji wa SDG’s kama ilivyokuwa katika utekelezaji wa malengo ya dunia MDG’s yaliyopita ili serikali iweze kufikia ngazi za chini kwa kuinua kipato cha wananchi kiendane na ukuaji wa uchumi wa nchi.
Mgeni rasmi Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli akitoa nasha wakati akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar ambao umefanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
 
Senga aliishauri serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendelea kuwashirikisha wananchi wa ngazi za chini katika kupanga na kutekeleza maendeleo yao katika maeneo husika ya wananchi.
 
“Changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kimataifa ili yaendane na mipango ya maendeleo ya serikali ni upungufu wa ushirikishwaji wa wananchi ama jamii husika na wengine hawafikiwi kabisa katika maeneo yao jambo linalotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka katika kutekeleza kwa vitendo Malengo ya Maendeleo Endelevu ya SDG’s”, alifafanua Senga.
 
Naye Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, Rogers Dhliwayo alisema Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s yanatakiwa yawekewe vipaumbele mbalimbali vya takwimu na tafti za kiuchumi katika maeneo tofauti ya jamii ili malengo endelevu yaweze kuwafikia walengwa.
 
Kwa upade wa washiriki wa mkutano huo kwa nyakati tofauti walisema kwamba mipango mbalimbali ya kimaendeleo inayopangwa na serikali inatakiwa kuwekewa vipaumbele kwa wananchi badala ya utekelezaji na tathimini kubakia ngazi za serikali kuu pekee.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha wakinakili mambo muhimu wakati mgeni rasmi (hayupo piichani) akitoa nasaha zake.
 
Walisema kwamba katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s ni lazima kutengeneza mpango mkakati wa mawasiliano wa masuala ya utamaduni, mila na desturi za jamii husika ambapo mipango hiyo inatakiwa kutekelezwa ili iwe rahisi wananchi kufahamu vizuri umuhimu wa mipango hiyo.
 
Washiriki hao walisema katika utekelezaji wa mipango hiyo ni lazima kuwepo na mikakati ya makusudi ya kuhakikisha changamoto ya umasikini uliokithiri unapungua kulingana na mikakati mbalimbali inayowekwa na vipaumbele vya kimataifa ili viweze kutekelezwa kwa vitendo na nchi husika.
 
Aidha wameshauri kwamba katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s ni lazima kuzingatia suala la serikali za mitaa, kutumia lugha nyepesi katika mawasiliano, kufanya marejeo katika maandiko ya baadhi ya waasisi wa kitaifa akiwemo Mwalimu Nyerere na kufanya utafiti juu ya matumizi sahihi ya Rasilimali.
Pichani juu na chini ni wadau wa sekta za maendeleo visiwani Zanzibar walioshiriki katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani humo ambao umefanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
 
Sambamba na hayo wamesema katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) ni lazima kuweka kipaumbele kwa makundi maalum ya watu wenye mahitaji maalum wakiwemo Watu wenye Ulemavu.
 
Warsha hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) ambapo imewakutanisha wadau mbalimbali kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
 
 
Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, Rogers Dhliwayo akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar.
 
Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) Ofisi ya Zanzibar, Anna Senga, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, mgeni rasmi Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha wakiwa meza kuu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto ya visiwani Zanzibar, Mauwa Makame Rajab akitoa maoni katika mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli wakisikiliza maoni ya wadau yaliyokuwa yakiwasishwa kwenye mkutano kuelekea utekelezaji wa SDGs.
Bw. Sefu Mwinyi kutoka Tume ya Mipango Zanzibar akiwasilisha maoni yake katika mkutano huo uliowakutanisha wadau wa sekta za maendeleo visiwani Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Khadija Juma (kushoto) akichangia hoja katika mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora visiwani Zanzibar, Asha Abdallah Ali.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.

UBUNGE WA OLE NANGOLE LONGIDO WATENGULIWA NA MAHAKAMA KUU ARUSHA

images 
Kesi iliyokuwa ikiunguruma kuanzia  Februari 29 ,2016 katika Mahakam Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii
Katika
shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt
Kiruswa  alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi
dhidi ya mbunge wa Longido Mh.Onesmo Nangole.
Akisoma hukumu
hiyo,Jaji Mwagesi  alisema kuwa mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa
na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.Katika shauri
hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo
Kutokana
na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa
pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka
mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;”Kutokana na kuzingatia
viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa
sheria,Natamka kwamba;
Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa
kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo
mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA MIKOA WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NA KUKUTANA NA MWENYEKITI WA GATES FOUNDATION MELINDA GATES

 MAF5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Mlingwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Zainab Telack kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  Wakuu wapya wa Wilaya mara baada ya kuwaapisha wakuu wapya watatu wa Mkoa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan watatu kutoka kushoto, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watatu kutoka kulia na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakwanza kushoto.
MAF9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wateule mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wateule mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF11 
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wateule  wakila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. 
MAF1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
MAF2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates watatu kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi

TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi
Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano la pamoja na wadau wa kodi nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi.
 
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi alisema wamekutanisha wadau hao wa kodi ili waweze kutoa maoni na kukubaliana kwa pamoja jinsi gani chombo hicho kitaweza kufanya kazi.
 
“Kutakuwa na chombo ambacho kitakuwa kinaratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi na lengo ni kupitia kongamano hilo wadau wa kodi wataweza kukubaliana kwa pamoja kuona ni jinsi gani chombo hicho kitafanya kazi,
Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililoandaliwa na TRA na kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi. (Picha zote na Rabi Hume – MO Blog)
 
“Unaweza kukuta kuwa mlipa kodi kwa sasa ndiyo anaumia au TRA ndiyo inaumia lakini chombo hicho kitaweza kusimamia na kuweka kila jambo sehemu sahihi kama linavyotakiwa kuwapo,” alisema Msangi.
 
Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo alisema kuwa chombo hicho kama kikianzishwa kitaweza kufanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na TRA ili kuhakikisha kuwa kinatoa na haki kati ya mlipa kodi na wakusanyaji wa kodi (TRA) bila kuumiza upande wowote kwani jambo hilo linawahusu wote.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo akitoa neno la ukaribisho katika ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika Bagamoyo, Pwani.
 
Alisema kupitia kongamano hilo wamekutanisha wataalam wa kodi, wahasibu, walipa kodi, wanasheria, washauri wa kodi na walimu wa kodi kutoka vyuoni ili kuweza kupata maoni ya pamoja na kupata maoni ya makubaliano ya pande zote ambayo yatatumika katika kuendesha chombo hicho.
 
Na Rabi Hume – MO Blog)
Baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo la siku moja lililofanyika Bagamoyo, Pwani.

DKT. NDUGULILE ATAKA MABUNGE KUSHIRIKISHWA KWENYE MPANGO WA “AFYA MOJA” (ONE HEALTH)

By Newsroom n June 29, 2016

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile(Mb) ameyataka Mataifa kushirikisha Mabunge katika kufanikisha mpango wa Usalama wa Afya Duniani (Global Health Security Agenda).
 
Akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia,, Dkt Ndugulile alisema, “Mabunge yanaweza kutoa mchango mkubwa sana kwenye utekelezaji wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani kwa kusimamia Serikali na kuhakikisha hatua zote muhimu zinatekelezwa; kutunga Sheria zitakazosimamia utekelezaji wa mpango huu pamoja na kuhakikisha mpango huu unapata fedha za kutosha kutoka kwenye Bajeti ya Serikali”.
 
Dkt Ndugulile alisema kuwa muingiliano wa shughuli za kilimo, mifugo na shughuli nyingine za kibinadamu zimesababisha baadhi ya magonjwa ya wanyama kuleta athari kwa binadamu na pia usugu wa madawa ya aina ya antibiotiki. Hivyo, kuna haja ya wadau wa sekta hizi kuwa na ushirikiano wa karibu chini ya mpango wa “Afya Moja” (One Health). 
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile (Mb) (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia.
Alisema kuwaIli mpango wa “Afya Moja” ufanikiwe in lazima maboresho yafanyike kwenye uratibu wa sekta mbalimbali ndani ya nchi na pia kuandaa mpango wa pamoja wa udhibiti na kushughulikia majanga.
 
Dkt Ndugulile aliyasema hayo kwenye mkutano wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani unaofanyika mjini Bali, Indonesia. Mkutano huu ulioanza tarehe 27 Juni unatarajia kuisha tarehe 30 Juni.
Dkt Ndugulile mbali ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mabunge Duniani (Inter Parliamentary Union) kuhusiana na masuala ya UKIMWI, Afya ya Wanawake, Vijana na Watoto.

Waziri Mkuu ahagiza wakuu wa Wilaya na Mikoa kutembelea Vijijini ili kujua matatizo ya wananchi.

index 
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa kufanya ziara katika maeneo yao hasa vijijini ili kujua matatizo ya wananchi wao kwa ukaribu na kuyapatia ufumbuzi.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo hii Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa  wakuu wa mikoa na wilaya waache kukaa maofisini mwao badala yake watembelee wananchi na hasa wale wa hali ya chini ili kujua matatizo yao ya Ardhi na kupatia ufumbuzi migogoro ya wafugaji na wakulima.
Pia Mhe.Majaliwa amewasisitiza wakuu hao kutambua kwamba majukumu waliyonayo ni makubwa na wananchi wana mategemeo makubwa juu yao na hivyo ni  budi wakatekeleza wajibu wao na kuhakikisha watanzania wanapata huduma zote za muhimu kwa kutumia elimu, uwezo, uadilifu, uaminifu na uwajibikaji walionao ili kufanikisha maendeleo kwa wananchi.
Aliongeza kuwa wakuu hao wana jukumu kubwa la kusimamia pesa za serikali pesa za miradi zinakokwenda katika halmashauri za wilaya zao na kukazia kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa yeyote ambaye hatofanya kazi zake kikamilifu.
Waziri mkuu amewaagiza wakuu wa Mikoa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa Wilaya ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maeneo yao kwani wananchi wana kiu ya maendeleo katika maeneo yao.

Makamu wa Rais awataka wakuu wa wilaya na mikoa kukamilisha zoezi la madawati kabla ya June 30.

index
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanamaliza zoezi la upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari.
Mhe. Suluhu ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha amewaagiza viongozi hao kusoma alama za nyakati kwa kuangalia makosa ya waliokuwepo kabla yao ili kuhakikisha hawarudii makosa yaleyale.
Mhe.Suluhu pia amesema kuwa Serikali haitaki kusikia wananchi wanalia njaa na hivyo wakuu wa wilaya wahakikishe chakula kinapatikana katika maeneo yao kwani hilo ni jukumu lao.
Aliongeza kuwa wakuu wa wilaya wana majukumu makubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za muhimu katika maeneo yao kwani wananchi wana mategemeo makubwa juu yao.
Aidha ameagiza wakuu wa Wilaya hao kufanya kazi karibu na Maafisa Tarafa ili kujua kero za wananchi na kuzifanyia kazi kwa kasi ili wananchi wafaidike na maendeleo yawafikie kwa haraka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene  ivi karibuni aliwaagiza wakua wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanatimiza agizo la Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayekaa chini kwa uhaba wa madawati kufikia June 30,2016.

Rais Magufuli Awataka wakuu wa Wilaya na mikoa kuchapa kazi.

index 
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuchapa kazi kwa bidii kwani viongozi hao ndio wawakilishi wa wananchi wa vijijini.
Mhe.Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kufanya kazi na kutimiza majukumu yao kwani wananchi wana changamoto nyingi,na wao waende kutatua matatizo ya wananchi walio maskini.
Aidha amewataka viongozi hao kutokuwa chanzo cha kutengeneza matatizo katika jamii na hivyo wasimamie haki na ukweli,wasiwe wala rushwa,wazingatie maadili na kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama zao,dini au kabila uku akiwataka kutekeleza waliyohaidi kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.
Pia amewataka viongozi hao kuweke mkazo katika kutatua kero za wananchi na kuwataka kutimiza kwa vitendo kwa kushirikiana na viongozi watakaowakuta katika maeneo yao waliyopangiwa.
Hata hivyo amewataka viongozi hao kusimamia mapato ya Serikali katika miradi yote kwenye maeneo yao ili kuhakikisha serikali inapata kodi ambayo itasaidia katika maendeleo ya Taifa hili.

Ijumaa, 27 Novemba 2015

ALIYEKUWA MGURUGENZI MSAIDIZI WA SHUGHULI ZA BUNGE BI.HELLEN MBEBA AFARIKI

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36), aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi-Shughuli za Bunge, kilichotokea ghafla leo Ijumaa tarehe 27/11/2015 wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu..

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI,AWAVUA GAMBA BAADHI YA MAAFISA TRA



Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maofisa watano na watumishi watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)kutokana na upotevu wa makontena
349 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 80.