SERIKALI YAPATA GAWIO LA SH. BILIONI 23 KUTOKA KAMPUNI ZA PUMA ENERGY, TIPER (T) NA NMB BANK PLC
Msajili
wa Hazina, Laurence Mafuru, akifafanua jambo wakati wa Hafla fupi ya
serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23
kutoka kwa Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo
imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma
(PICHA NA BEN MWAIPAJA KAIMU MSEMAJI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO)
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akipokea hundi
kifani yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.5 kutoka kwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Puma Energy Dkt. Ben Mosha, wakati wa
Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya
shilingi Bilioni 23 kutoka kwa Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC
Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury
Squire) Mjini Dodoma
Naibu
Waziri wa Nishati na Mdini Dk. Medard Kalemani, akizungumza jambo
wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye
thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka kwa Kampuni za Puma Energy, Tiper
(T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina
(Treasury Squire) Mjini Dodoma
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango(Mb), (Katikati) akimwelekeza
jambo Msajili wa Hazina Laurence Mafuru, wakati wa Hafla fupi ya
serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23
kutoka Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo
imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini
Dodoma
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika, akipokea
mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Bil. 2.0 kutoka kwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tiper (T), Prof. Abdulkarim Mruma, wakati wa
Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya
shilingi Bilioni 23 kutoka Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank
PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury
Squire) Mjini Dodoma
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb)
akizungumza jambo wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za
Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka Kampuni za Puma
Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika
ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini Dodoma
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango(Mb), (Katikati) akinyoosha dole
gumba kuashiria “mambo safi”, wakati akipokea hundi ya shilingi Biln
16.5 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker,
wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye
thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka Kampuni za Puma Energy, Tiper (T)
na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina
(Treasury Squire) Mjini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………………………………………
Serikali imepata gawio la
shilingi Bil. 23 kutoka Kampuni tatu za NMB Bank PLC, Puma Energy na
Tiper (T) ikiwa ni faida iliyotokana na biashara iliyofanyika katika
kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016, ambazo imewekeza hisa zake kati ya
asilimia 31 na 50.
Mfano wa hundi zenye thamani ya
kiasi hicho cha fedha zimekabidhiwa kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Philip Mpango, katika Ofisi za Hazina Ndogo Mjini Dodoma, leo Juni 9,
2016
Kampuni ya kwanza kukabidhi gawio
(dividends) ni Puma Energy, inayojihusisha na biashara ya kuuza mafuta,
ambayo serikali ina hisa zake asilimia 50 iliyokabidhi mfano wa hundi
yenye thamani ya shilingi Bil. 4.5 (Bilioni 4 nukta 5) baada ya kampuni
hiyo kupata faida ya shilingi Bil. 9 katika kipindi kinachoishia Desemba
mwaka jana
Kampuni ya Tiper (T) inayofanya
biashara ya uhifadhi wa mafuta (storage), ambayo serikali ina hisa ya
asilimia 50 pia, imekabidhi gawio la shilingi Bil 2.0 (Bilioni 2 nukta
0) na kufuatiwa na Benki ya NMB PLC, iliyomkabidhi Waziri wa Fedha Dk.
Philip Mpango, hundi kifani yenye thamani ya shilingi Bilioni 16.5
(Bilioni 16 nukta 5)
Serikali imepata kiasi hicho cha
fedha kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, inayosimamia Mashirika,
Taasisi za Umma na Kampuni zenye hisa na serikali.
Akizungumza baada ya kupokea
hundi hizo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amezishukuru
kampuni hizo kwa kuiwezesha serikali kupata kiasi kikubwa cha fedha
zitakazotumika kuwahudumia wananchi.
“leo ni siku yangu ya furaha sana
kwa kupata kiasi kikubwa cha fedha kiasi hiki ikiwa ni siku moja tu
tangu niwasilishe Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni hapa Mjini Dodoma”
aliongeza Dkt. Mpango
Amemwagiza Msajili wa Hazina,
Laurence Mafuru, kuhakikisha kuwa kampuni zote ambazo serikali ni mbia
zianze kulipa gawio kwa serikali na kuacha visingizio vya kutangaza
kupata hasara kila mwaka wakati hawafungi biashara zao.
“Naomba vyombo vinavyohusika na
ukusanyaji wa mapato ya serikali pamoja na Msajili wa Hazina
kuzifuatilia na kuzikagua kampuni ambazo serikali ina hisa ili kubaini
ukweli ni kwanini hazitoi gawio zikisingizia kupata hasara kwenye
biashara wakati hawafungi biashara hizo” Alisisitiza Dk. Mpango
Dk. Mpango pia amevitaka vyombo
vya dola kufanya uchunguzi, ili kubaini mianya ya upotevu wa mafuta
bandarini na kuagiza wale wote walihusika na upotevu huo wachukuliwe
hatua.
” Haiwezekani wajanja wachache
wanafaidika halafu wananchi wanyonge wanalala chini hospitalini,
Nilisema jana na leo narudia yeyote anayetukwamisha kwenye maendeleo ni
msaliti lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria bila huruma,”
alisema.
Awali Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dk. Medard Kalemani, amezipongeza kampuni hizo kwa kutoa gawio
hilo na kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango,
kuwa gawio litaongezeka kwa kasi kubwa katika miaka ijayo ili kuiwezesha
serikali kuwa na uwezo zaidi wa kuwahudumia wananchi.
“Mwaka 2014 tulipata gawio la Sh
bilioni 3 kutoka Kampuni ya PUMA Energy, mwaka huu tumepata bilioni 4.5
ni matarajio ya Serikali kwa mwendo huu mwakani tunaweza kupata bilioni
6″ alisema Dkt. Kalemani.
Alitoa wito pia kwa kampuni
nyingine zenye ubia na Serikali ambazo hazitoi gawio zianze sasa kutoa
akieleza kuwa mantiki ya gawio ni kwamba kampuni inafanya kazi na
inapata faida, inapokuwa haitoi gawio mantiki yake ni kwamba kampuni
inafanya kazi haipati faida.
“Lakini ni vigumu kuamini kama
kampuni hazipati faida kwa mfululizo wa miaka 10 na inafanya kazi, sisi
tunaamini wanapata faida, na zipo kampuni nyingi ambazo si busara
kuzitaja hapa zinadai kupata hasara kila mwaka,” alisema.
Kuhusu upotevu wa mafuta
bandarini, Dk. Kalemani alisema tatizo hilo hivi sasa limedhibitiwa,
baada ya Serikali kuanzisha chombo maalumu kinachoratibu na kudhibiti
upotevu huo.
Alikuwa akijibu changamoto
iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Puma Energy, Dkt. Ben Moshi,
aliyeelezea kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 kampuni hiyo imepata
hasara ya Dola za Marekani milioni 1.4 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni
2.5 kutokana na upotevu huo wa mafuta.
Kwaupande wake, Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tiper (T), inayojihusisha na uhifadhi
wa mafuta, ambapo amesema tangu mwaka 2010, kampuni hiyo imetoa gawio la
shilingi Bil. 6.4 kwa serikali na kuahidi kuwa gawio hilo litaongezeka
siku za usoni.
Naye Mkurugenzi wa Benki ya NMB,
Ineke Bussemaker, amesema kuwa benki yake inajisikia fahari kubwa
kugawa faida iliyopata katika biashara zake kwa mbia wake ambaye ni
serikali.
Amesema kuwa pamoja na serikali
kuwa mbia kwa hisa ya asilimia 31.8, lakini pia ni mteja mkubwa wa benki
hiyo ambayo hurudisha faida ya uwekezaji kwa wananchi kupitia gawio
hilo na kutoa wito kwa watanzania kuitumia benki hiyo kuweka amana na
kukopa
Hafla hiyo imehudhuriwa pia na
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ambaye ametoa
wito kwa wawekezaji wakiwemo wale wanaofanya biashara zao kwa
kushirikiana na serikali kufanyakazi zao kwa uaminifu kwa kutangaza
faida wanazopata kihalali ili serikali iweze kupata mapato yake
yatakayosaidia kuboresha maisha ya wananchi
Naye Msajili wa Hazina, Laurence
Mafuru, ameahidi kuyafuatilia na kuyasimamia mashirika yote ya umma na
yale ambayo serikali imewekeza, ili kuhakikisha kuwa hawakwepi kulipa
gawio ili kuiwezesha serikali kupata mapato yake
Imetolewa na
Benny Mwaipaja
Kaimu Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni