Jumatano, 15 Juni 2016



Nataka Kufanya kazi na Chamereone

Na Raymond Urio, Dar
Msanii na Muimbaji wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Juma Bakari  ‘Juma B’ ametambulisha rasmi wimbo  weake Mpya unaoenda kwa jina la “Mtoto Mlimbwende” aliemshirikisha Mwanamuziki Garinya Six.


 Msanii wa Kizazi Kipya Juma Bakari ' Juma B'

Msanii huyo ambae amepanga kuleta Mapinduzi katika soko la Muziki nchini, amewaomb amashabiki wapokee vyema kazi zake ambazo ameshafanya na wasanii wanaotamba nchini.


Akizungumza na Mwandishi wa Blog ya Makanya West, Bakari alisema kuwa, anaowaomba mashabiki waweze kumpokea kwa mikono miwili kwa kuwa ndio mara ya kwanza kuingia katika soko la Muziki nchi.


“Nawaomba mashabiki wote wazipokee kazi zangu ambazo zimetoka na teyari baadhi ya nyimbo ziko Sokoni ni wao kuchukua na kuzisikiliza, alisema Bakari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni