WIZARA YA AFYA KUFANYA UZINDUZI WA KONDOMU MPYA MKOANI MWANZA.
Baada
ya juzi Agost 30,2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, kuzindua aina mpya ya Kondomu iitwayo Zana Kondomu mkoani
Mbeya, Uzinduzi kama huo unatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza Septemba
05,mwaka huu.
Afisa
Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni (pichani), jana
alisema mkoa wa Mwanza unatarajia kupokea ugeni kutoka wizara hiyo ambao
utajumuisha wataalamu mbalimbali wa afya watakaokuwa wakitoa semina na
elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia vyombo vya habari, wakielezea
juu ya uzinduzi wa kondomu hiyo.
Alisema
miongoni mwa dhumuni la kuzindua aina hiyo mpya ya Kondomu, ni kusaidia
katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukwimwi ambapo
Wizara itakuwa ikigawa bure kondomu hizo zenye ubora kwa wananchi, kote
nchini.
Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni
Baadhi ya Wanahabari mkoani Mwanza, wakimsikiliza Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni