Jumatano, 31 Agosti 2016

UONGOZI WA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO KATIKA ENEO LA MWENGE WAPINGA OPERESHENI UKUTA


2
Mwenyekiti wa  wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika halimashauri ya Kinondoni,Bw  Omary Hamis (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) akipinga wafanya biashara wake wasi kubali kurubuniwa na wanasiasa katika mambo ambayo hayana faida kwao (kulia) Sharifu Hasan.
1
Mwenyekiti wa  wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika halimashauri ya Kinondoni,Bw  Omary Hamis (katikati) akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo, kushoto ni Katibu wa Ulinzi Shirikishi wa Wafanyabiashara wa eneo hilo, Dick Ponda, na kulia  Sharifu Hasan.
Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam
…………………………………………………………………………………………….
MWENYEKITI wa wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika halimashauri ya Kinondoni, Omary Hamis amewataka wafanya biashara wake wasi kubali kurubuniwa na wanasiasa katika mambo ambayo hayana faida kwao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam , alisema maranyingi vijana ndio wamekuwa wakishawishiwa kuandamana hivyo wao meona hakuna umuhimu wa kuandamana kwani kufanya hivyo hakuna faida kwao.
“Maranyingi vijana wamekuwa wa kishwawishika na wana siasa kuandamana kitu ambacho siyo chamsingi kwetu kama ambavyo tunashawishiwa tuandamane Septemba mosi mwaka huu eti kisa kuna Oparesheni Ukuta, hivi kwani huo ukuta unafaida gani kwetu, ifahamike kuwa hii nchi ni moja, Taifa letu n moja sisi ni wamoja hivyo tusikubali kufanya maandamano yasiyo na tija kwetu,” alisema Hamis.
Aliongeza kuwa Rais John Magufuli ameonesha nia ya dhati ya kupambana na maadui watatu amabao ni Maradhi, Ujinga na Umasikini hivyo hakuna sababu ya kuacha kumungamkono kutoka na juhudi anazo zifanya za kujenga Taifa hasa kwa kuwatetea wanyonge.
Naye Katibu wa Ulinzi Shirikishi wa Wafanyabiashara wa eneo hilo, Dick Ponda alisema Mfanyabiashara yoyote yule na vijana wote nchini atakama ni mwanachama wa Chadema au chama chochote kile asikubali kushwawishika kuandamana na Oparesheni ukuta kwani Rais wa nchi amekataza maandamano, na kufanya hivyo kutasabisha madhara makubwa kwao.
Alisema umefika wakati sasa vijana kujituma kwa bidii katika kufanya kazi, muda uliopo ni wakufanya kazi na wala si siasa kama baadhi ya vyama wanavyo fanya, Rais John Magufuli haangali chama katika utendaji wake hivyo kila mtu anapaswa kuweka maswala ya chama chake pembeni.
Kwa upande wake mmoja kati ya Wafanyabiashara hao, Fadhili Leuteni alimpongeza mwenyekiti wao kutokana na ujasili wake wakuwakemea wafanyabiashara wa eneo hilo.
“Mwenyekiti wetu pamoja na viongozi wake wapo sahihi kwasabu maranyingi sisi ndio tumekuwa tukitumiwa katika mambo ya uchochezi, hivyo na waomba wezangu wasikubali kulubuniwa na wanasiasa kwani tutapata madhara makubwa ni vyema kujiepusha,” alisema.

Baraza la ushauri latoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda kwenye insha


TOL1
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  anayesimamia sekta Mawasiliano mhandisi Dkt. Maria Sasabo kushoto akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano, kulia ni Katibu wa Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano  Bi. Mary Shao Msuya.
TOL2
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Bw. Stanley Mwabulambo akimkaribisha mgeni rasmi  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria Sasabo kuzungumza na wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano  
TOL3
Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu Bw. Omari Abbas kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Ualimu (DUCE) akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt.   Maria Sasabo.
TOL4
Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za sekondari Bw, Ramadhani Mohamed kutoka Shule ya sekondari ya Kibasila  akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.
TOL5
Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za Msingi  Jane Michael Andrew  kutoka shule ya msingi ya Mbuyuni akipokea zawadi ya cheti ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.

SERIKALI IMEJIDHATITI KUSIMAMIA RASILIMALI ZA NCHI IPASAVYO


Profesa Jumanne Maghembe-July1-2014
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe.
…………………………………………………..
Na Hassan Silayo, MAELEZO
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa serikali imepiga marufuku biashara ya kusafirisha wanyama hai nje ya nchi mpaka pale itakapowekwa misingi mizuri ili nchi iweze kunufaika na biashara hiyo.
Prof. Maghembe ameyasmea hayo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC 1 ambapo alisema Serikali iliamua kuangalia upya utaratibu huo wa kuuza wanyama hai na kuamua kusitisha biashara hiyo hadi pale taratibu na misingi mizuri ya biashara hiyo itakapowekwa.
“Ni kweli kulikuwa na utaratibu wa kuuza wanyama hai nje ya nchi bila kuiwezesha nchi kupata faida yoyote ile, hivyo kwa sasa kama nchi tumeamua kupiga marufuku biashara kwa maslahi ya taifa”.
“Haiwezekani uuze wanyama hai nje halafu anayenufaika ni yule anayenunua na kuiacha nchi bila faida yoyote ya uwepo wa maliasili hiyo, hivyo kama nchi tumeamua kupiga marufuku biashara hiyo hadi pale misingi mizuri ya kibiashara itakapowekwa na kuiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake, na nisisitize kwa sasa hata Chawa wa Tanzania hataweza kusafirishwa nje ya nchi”. Alisema Prof. Maghembe.
Aidha, Prof. Maghembe alisema kuwa kwa sasa Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na ujangili wa wanyama pori kama Tembo na Faru ikiwemo kukamata watu wote wanaohusika katika biashara hiyo na mpaka sasa wameshakamata  baadhi ya watu akiwamo mwanamama anayejiita malikia wa pembe za ndovu ambaye alikuwa kinara katika biashara hiyo.
Prof. Maghembe aliongeza kuwa hatua hiyo imeonesha mafanikio kwani kwa kipindi cha hivi karibuni soko la mauzo ya pembe za ndovu nje nchi hasa bara la Asia ambao ndio walikuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa hizo yameshuka na hatua hiyo inatokana na mikakati iliyowekwa na Serikali.
Akizungumzia wizi katika mazao ya misitu Prof. Maghembe alisema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kupambana na wizi wa mazao ya misitu na imekubaliwa kuwa iwapo gari litakamatwa likiwa na mazao hayo bila kuwa na kibali, Serikali itataifisha gari hilo na wahusika watashtakiwa kama wahujumu uchumi.
Pia Prof. Maghembe alisema kuwa kwa sasa utawekwa utaratibu wa magari yote yanayobeba mazao ya misitu kusafiri mchana kwenye gari lililo wazi ili kurahisisha ufuatiliaji na udhibiti wa wizi huo.
Serikali imeahidi kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki kwenye vijiji vilivyo pembezoni mwa misitu ili kuweza kudhibiti uchomaji moto kwenye kwenye maeneo hayo hali itakayowezesha pia utunzaji wa mazingira.

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK.


Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa
maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho
kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu
Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)  Pascal Shelutete
akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua   litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune
Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa
habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya
kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.
Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
Septemba mosi .
Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
Septemba mosi . 
 
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali,Mbeya . 
 
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio  la kupatwa  kwa jua
linalotarajia kuonekana Septemba mosi  mwaka huu kufungua lango la Ikoga
katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI
ya Taifa ya Ruaha 
Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya
kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction
ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Pascal Shelutete  anasema kuongezeka kwa
geti la Ikoga ni  fursa kubwa ya
kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa  eneo la Ihefu
linakivutio kikubwa cha wanyama
wa aina mbalimbali .
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema
Wilaya hiyo   ina vivutio vingi, hivyo
amewataka  wananchi watakaofika kuangalia
kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio
vilivyopo Wilayani humo.
Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi
majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga
Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .

WAZIRI NAPE AKUTANA NA UMOJA WA VYAMA VYA WAALIMU WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA(SATO)

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimia na Rais wa Chama
cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mkoba walipokutana katika ufunguzi wa
mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa
Afrika (SATO)yaliyofanyika Agosti 30,2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye akimsikilza Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian
Mkoba walipokuwa wakijadiliana maswala mbalimbali ya kimichezo katika ufunguzi
wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa
Afrika(SATO) uliofanyika Agosti 30,2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye (wa pili kushoto) akizungumza na viongozi wa Umoja wa Vyama vya
Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) katika ufunguzi ya mashindano ya
michezo ya Umoja huo uliofanyika Agosti 30,2016.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Yahya
Msugwa(kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto) walipokutana katika ufunguzi wa
mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa
Afrika (SATO) uliofanyika Agosti 30,2016.
Rais wa Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini
mwa Afrika(SATO) Bw. Henry Kapenda akielezea jambo kwa Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto) walipokutana
katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi
za Kusini mwa Afrika (SATO) uliofanyika Agosti 30,2016.
 
PICHA na  Raymond Mushumbusi WHUSM

WAZIRI PROF.MBARAWA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA JAPANI KUJADILI FURSA MBALIMBALI KATIKA SEKTA YA MIUNDOMBINU


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na
Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam kuajadili
fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu. Kulia kwake ni
Rais wa
  chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akimuonyesha Rais
wa
  chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano na ujumbe wake taarifa ya maendeleo ya Miundombinu
nchini, 
 walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam.
 Rais wa chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano (wa nne kulia)  akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es salaam kuajadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa
Rais wa
  chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano, wakati Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea Ofisini kwake
kujadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa
Rais wa  chama cha maendeleo ya Uchumi wa Afrika Bw. Tetsuro Yano wakati Ujumbe kutoka Japani ulipomtembelea Ofisini
kwake kujadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya Miundombinu.
PICHA NA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (W-UUM)

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA TAASISI YA AFRICA MATTER LIMITED YA UINGEREZA MHE. LYNDA CHALKER


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimkaribisha kuketi  Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimsindikiza Mwenyekiti wa Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya  mzungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016
 “Hapa kazi tu…” anaonekana kusema Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya  mzungumzo yake na   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto M. James

DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

   4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Hassan Khatib Hassan  kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika  hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipeana mkono wa shukurani na Nd,Hassan Khatib Hassan,baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika  hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ,katika  hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini hati ya kiapo ya ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo  ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
1
Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ walihudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi, walioteuliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
2
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
3
Baadhi ya Mawaziri wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi katika taasisi mbali mbali walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
[Pica na Ikulu.] 31/08/2016.