Wizara ya Afya yapokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro
(kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini
Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro
(kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini
Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye
thamani ya shilingi bilioni 1.4 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutoa
chanjo kwa akina mama na watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali nchini.
Akiongea na waandishi
wa habari Wizarani hapo, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila
ameeleza kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia uhifadhi wa chanjo katika
mikoa mbalimbali pamoja halmashauri nchini.
‘’Ni msaada mkubwa tulioupata
toka WHO na nina amini kuwa utatusaidia sana katika kufanikisha suala la
chanjo kwa akina mama na watoto nchini na pia tunaamini wataendela
kushirikiana na Wizara ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea’’,
alisema Dkt. Rusibimayila.
Ameongeza kuwa, kwa sasa vituo
vipya vinavyofunguliwa nchini vikiwemo vile ambavyo havikuwa na majokofu
vitakuwa na uwezo wa kupata vifaa hivyo kama vile majokofu na vifaa
vingine vya tiba ili huduma za chanjo ziweze kutolewa katika kila kituo
nchini.
Akikabidhi vifaa hivyo Wizarani
hapo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.
Rufaro Chatoro amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi
bilioni 1.4 ni pamoja na majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa
ajili ya kutolea chanjo.
Kwa upande wake Mratibu Chanjo
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana
Emmanuel Yohana ameeleza kuwa, majokofu hayo pia yatapelekewa katika
wilaya ambayo yana upungufu wa majokofu pamoja na vituo vipya kwa ajili
ya kupunguza umbali kwa wagonjwa wa chanjo na pia ni moja ya kuweka
huduma karibu na wananchi nchini.
Aidha, ameongeza kuwa spesimeni
za polio na surua zilizotolewa na WHO zitapalekwa pia katika vituo kwa
jili ya kuchukua damu kwa ajili ya vipimo na kuletwa Dar es Salaam kwa
uchunguzi zaidi wa maabara.
‘’Wanufaika wa huu msaada
kutoka WHO ni wananchi wote wa Tanzania kwani utaenda katika vituo vyote
vya chini zikiwemo Zahanati’’, alisema Yohana.
Kupitia wadau mbalimbali Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea
kushirikiana na wadau hao katika kutafuta vifaa tiba mbalimbali kwa
lengo la kuhakikisha kuwa sekta ya afya nchini inaimarika kwani Tanzania
kwa sasa imeweza kudhibiti polio kwa kiasi kikubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni