Jumatatu, 30 Mei 2016


Na Saleh Ally
KWANZA anza kwa kujiuliza kama ungekuwa wewe ndiye Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone ungejisikiaje? Hakika ni maumivu makali ya moyo.

Lazima ungehisi au kuamini hauna bahati hata kidogo na hasa linapofikia suala la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ndani ya miaka mitatu, Simeone amekiongoza kikosi chake kucheza fainali mara mbili dhidi ya timu moja.

Fainali ya kwanza msimu wa 2013/14 ilikuwa dhidi ya Real Madrid kama ile ya 2015/16.  Zote mbili wamepoteza, moja wakianza kufunga Madrid wakasawazisha, ya usiku wa kuamkia jana wakaanza kufungwa, wakasawazisha na kung’olewa kwa mikwaju ya penalti 5-3.

Mtu asiye na bahati kwa Lugha ya Kihispania anaitwa sin suerte. Unaweza ukampa jina hili Simeone raia wa Argentina anayeonekana ni mtu asiyekata tamaa na kila kitu.

Simeone ni kocha aliyeshinda makombe kadhaa makubwa na muhimu akiwa na Atletico Madrid. Amechukua ubingwa wa La Liga, Copa del Rey, Super Cup Hispania, Europa Cup na Uefa Super  Cup pia.
Si mgeni wa makombe tokea akiwa mchezaji hadi kocha. Lakini kombe pekee ambalo linaonekana kumteleza kila anapojaribu ni lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Rekodi yake na kikosi cha Atletico Madrid inamfanya aonekane mmoja wa makocha bora kabisa kuwahi kuifundisha timu hiyo aliyowahi kuichezea pia.

Tokea ajiunge nayo mwaka 2011, ameiongoza katika mechi 260. Ameshinda 164, sare 52 na kapoteza 44, hii inamfanya awe na wastani wa juu kabisa wa 63.1% ya ushindi. Huu ni wastani wa juu kwa kocha anayefundisha timu kubwa zinazoshiriki michuano yenye ushindani wa juu.


Ukiachana na rekodi za mafanikio yanayopatikana baada ya mchezo, angalia mchezo wenyewe. Mfano, fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Madrid pale jijini Milan, Italia.

Kikosi chake kilicheza vema zaidi, ingawa mwenyewe mwisho alisisitiza kwamba kuna mambo walizidiwa ambayo ndiyo yalifanya wapinzani wao mwisho wabebe ubingwa huo mbele yao.

Simeone anakubali kuwa ana maumivu ya moyo, huenda maumivu hayo yametambaa kwa mashabiki wengi wa soka duniani kote wakiwemo wale ambao si mashabiki wa Atletico Madrid, lakini wanaumia kwa kuwa wanajua kocha huyo Muargentina anaifanya kazi yake kwa ufasaha.

Wanajua kikosi chake kufikia kucheza namna hiyo ni mtu anayejituma, anayefanya jambo kwa juhudi kubwa lakini inaonekana mafanikio yanamkimbia hasa katika Ligi ya Mabingwa.

Kabla ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa jijini Milan, Ronaldo de Lima alipata nafasi ya kumzumngumzia Simeone ambaye alicheza naye timu moja wakiwa Inter Milan ya Italia pia.

Ronaldo alianza kwa kupinga tabia ya Simeone kupandikiza hasira za Kiargentina kwa wachezaji wake, akisema wanakuwa wajeuri na wakatili. Lakini mwisho, akasema ni wagumu kushindika na kocha huyo ni kati ya makocha bora kabisa duniani. 


Kwenye kutengeneza jambo mengi yanatokea, lakini mwisho ni matokeo bora. Simeone amekuwa akiyapata lakini tatizo kubwa ni Ligi ya Mabingwa.

Kinachovutia kwa huyu jamaa ni maneno yake ya mwisho kuhusiana na kuonekana hana bahati ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Sitaki kuonyesha machungu yangu kwenu, lakini najua naumia kiasi gani kufika hapa mara mbili lakini sijarudi nyumbani na kombe. Hakuna ambaye angeweza kufurahia.

“Utaona, wachezaji wamepambana hadi mwisho, wamecheza mechi nyingi sana ndiyo maana dakika 15 za dakika 30 za nyongeza, kila mmoja alionekana ameisha kabisa.

“Najua hatukufika hapa kwa bahati hata kama kweli tuna bahati mbaya. Hatuwezi kuishia hapa, niwaahidi ninabaki Atletico na kwa mara nyingine tunataka kufika fainali ili tuiondoe bahati mbaya,” anasema.

Wengi wanaamini Atletico au Simeone wana bahati mbaya na kombe hilo. Kutokana na wanavyojituma watu wanawaonea huruma, vyote viwili anavikataa.

Utagundua kuwa Simeone si mpiganaji wa muda mfupi, si muoga, si anayetaka kuonewa huruma na anachoamini ni kurejea na kupigana tena ili wafike fainali kumaliza makosa ya fainali mbili zilizopita.

Hakuna ubishi, siku wakifanikiwa kuingia fainali tena, kutwaa kombe hilo halitakuwa na mjadala. Lakini utaona namna kamanda anavyopaswa kuwa, hata kama kaumia anaonyesha bado mapambano yanaendelea.

Simeone anaficha maumivu yake ili kuinua mioyo ya wachezaji wake lakini pia anafuta hisia za wao hawana bahati na Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Kama yeye akikubali, maana yake vijana wake wakati mwingine watakuwa hawana sababu ya kulipigania.

Hii ni falsafa ya kiongozi sahihi ambaye maisha yake yote hachoki kupambana na hakati tamaa kwa kuwa hataki kuonewa huruma. Kuhurumiwa ni falsafa ya kusaidiwa au kubebwa, Simeone hataki na tayari amerejea tena kwenye mapambano.


MAFANIKIO YA SIMEONE
AKIWA MCHEZAJI 
Atletico Madrid
La Liga (1): 1995–96
Copa del Rey (1): 1995–96

Inter Milan 
Uefa Cup (1): 1997–98

Lazio (4)
Serie A (1): 1999–2000
Coppa Italia (1): 1999–2000
Supercoppa Italiana (1): 2000
UEFA Super Cup (1): 1999

TIMU YA TAIFA
Argentina (4)
Kombe la Mabara Fifa (1): 1992
Copa America (2): 1991, 1993
Artemio Franchi (1): 1993
Medali ya Fedha Olimpiki (1): 1996

KAMA KOCHA
Estudiantes de La Plata (1)
Ubingwa Argentina (1): Torneo Apertura 2006

River Plate (1)
Ubingwa Argentina (1): Torneo Clausura 2008

Atletico Madrid (5)
La Liga (1): 2013–14
Copa del Rey (1): 2012–13
Supercopa de Espana (1): 2014
UEFA Europa League (1): 2011–12
UEFA Super Cup (1): 2012

BINAFSI 
Kocha Bora wa Mwaka La Liga (2): 2012–13, 2013–14
Tuzo ya Miguel Munoz (1): 2013–14
Kocha Bora wa Mwezi La Liga (2): Oktoba 2013, Novemba 2015



Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amerusha kombora kwa wapinzani wake na kusema wanamuonea wivu lakini atabaki kuwa namba moja.

Hata hivyo, Ronaldo ambaye alifunga penalti ta mwisho wakati Madrid ikiishinda Atletico Madrid na kubeba kombe hilo kwa penalti 5-3, hakueleza moja kwa moja anamlenga nani.

Ronaldo ameyasema hayo wakati wa hafla ya mashabiki wa Madrid kulipokea kombe la ubingwa wa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.


Ronaldo sasa ameshinda kombe hilo mara tatu pia ametwaa tuzo tatu za mwanasoka wa dunia.

Raia huyo wa Ureno ameendelea kusisitiza ataendelea kubaki namba moja miongoni mwa wanasoka bora kwa kipindi hiki.






RAIS WA ZANZIBAR MH. DK. SHEIN KATIKA ZIARA YA KICHAMA KISIWANI PEMBA

MIC2Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Wete Abrahmani Makame Shehe alipokuwa akisoma risala ya wilaya wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipozungumza na Wanachama wa CCM Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na ushindi katika uchaguzi wa marudio wa mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
MIC1Baadhi ya WanaCCM wakitetemka gari walipofika Viwanja vya Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipozungumza na Wanachama wa CCM Wilaya hiyo leo kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na ushindi katika uchaguzi wa marudio wa mwezi machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
MIC3Viongozi wa Mashina,Wenyeviti na Makatibu wa maskani wakiwa ni Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Wete wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipozungumza na viongozi hao leo wakati alipofika katika ukumbi wa  Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba  kuwapongeza na kuwashukuru kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 30/05/2016.
MIC4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein akipokea risala ya Wilaya kutoka kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Wete Abrahmani Makame Shehe katika mkutano wa Viongozi wa Chama Wilaya ya Wete uliofanyika leo katika ukumbi wa skuli ya Kiislamu Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
MIC5Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete  Bw.Kombo Hamadi Yussuf alipokuwa akiwasalimia Viongozi wa CCM wa Mashina,Matawi na Maskani waWilaya ya Wete  wakati wa Mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipowashukuru wana CCM wa Wilaya hiyo kwa ushindi katika uchaguzi wa marudio wa Mwezi Machi mwaka huu uliofanyika leo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu Wilaya ya Micheweni Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
MIC6Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kasakzini Pemba Khadija Nassor Gulam  alipokuwa akizungumza machache na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa wakati wa Mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein alipowashukuru wana CCM wa wilaya hiyo kwa ushindi katika uchaguzi wa marudio wa Mwezi Machi mwaka huu uliofanyika leo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu Wilaya ya Micheweni Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
MIC7Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipokuwa akiwasalimia Viongozi wa CCM wa Mashina,Matawi na Maskani wa Wilaya ya Wete  walipohudhuria katika mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza Viongozi hao uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein leo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu ya kiuyu Wilaya ya michweani Mkoa wa Kaskazini Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.
MIC8Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa katika mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza Viongozi wa CCm wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu ya kiuyu Wilaya ya Michweani Mkoa wa Kaskazini Pemba,[Picha na Ikulu.]30/05/2016.

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imekanusha taarifa iliyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya gari linalodaiwa kuwa la DAWASCO lenye namba za usajili T 369 BUZ ambalo liliparamia kituo cha mabasi cha Mbuyuni kilichopo maeneo ya Namanga Oysterbay na kujeruhi watu watatu.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro amesema kuwa gari hilo sio mali ya Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam, bali ni moja ya gari linalomilikiwa na watu binafsi   ambao wanasaidiana na Dawasco katika kusambaza huduma ya maji maeneo ambayo huduma hiyo bado haijafika kwa kutumia magari makubwa ya kusambaza Maji (maboza) ambayo yamesajiliwa na kuwekwa nembo ya Dawasco.

“Gari hili sio mali ya Dawasco, bali limesajiliwa na Dawasco na kuwekewa viambatanisho vyote muhimu  ili kusambaza huduma ya Maji maeneo ambayo mtandao wa Maji haujafika haujafika” alisema Lyaro.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Dawasco ilianza zoezi maalum la kusajili visima pamoja na magari yote makubwa ya kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es salaam, ambapo tayari magari makubwa takribani 256 ya kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es Salaam yamekwisha sajiliwa.
Dawasco inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari kuzingatia taratibu za kazi kwa  kuandika taarifa zenye uhakika na ukweli ili kuepuka upotoshaji wa habari kwa wananchi.
Everlasting Lyaro
Kaimu Meneja uhusiano- Dawasco
022-2194800 au 08001164
Dawasco Makao Makuu
indexMratibu Miss Chang’ombe 2016 kutoka  Kampuni ya SG Entertainment Adam Hussein(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa Mashindano ya Urembo Kitongoji cha Chang’ombe yanayotarajiwa kuzinduliwa Juni 02, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo Victor Mkumbo na Kulia ni Meneja Masoko Geofrey Msala.(Picha Na: Lilian Lundo)
 Kampuni ya SG Entertainment kuzindua mashindano ya urembo ya Miss Chang’ombe Juni 2, 2016 katika Ukumbi wa MPOA AFRIKA uliopo Davis Corner Tandika jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo Victor Mkumbo  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza  kuwa  watakaoshiriki mashindano hayo ni wakazi wa Chang’ombe na Temeke peke yake.
“Washiriki wa mashindano haya ni wakazi wa Chang’ombe na Temeke, nje ya hapo haturuhusu mtu kutoka eneo lingine kushiriki, lengo ikiwa ni kuwapa fursa wakazi wa maeneo haya”,” anasema Mkumbo.
Kwa upande wake Mratibu wa Miss Chang’ombe 2016 Adam Hussein anasema kwamba nafasi za warembo kushiriki bado zipo na fomu za kujiunga zinapatikana CDS PARK(TCC Club) Chang’ombe, MPOA AFRIKA Davis Kona na duka la nguo CHILU Latest Wear Temeke Mwisho kwa gharama ya shilingi 5,000 tu.
Aliongeza kuwa fainali ya mashindano hayo itafanyika Julai 21, 2016 katika viwanja vya CDS Park(TCC Club) Chang’ombe ikisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Galatone ,mwadada  Chemikal.
Washindi watano kutoka Kitongoji cha Chang’ombe wataungana na warembo kutoka vitongoji vya Kigamboni na Mbagala ili kutafuta warembo wa Temeke watakao wakilisha katika mashindano ya kitaifa ya kumtafuta mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Mrembo wa Dunia mwaka huu.