TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MZFA
Shirkisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Mpira wa
Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti
mstaafu wa MZFA na makamu mwenyekiti wa FAT Silvanus Makalu Ngofilo
aliyefariki dunia juzi jijini Mwanza.
Katika salamu zake, TFF imewapa
pole familia ya marehemu Ngofilo ndugu, jamaa, marafiki, wadau wa mpira
wa miguu kanda ya Ziwa na kusema Shirikisho liko pamoja nao katika
kipindi hiki cha maomblezo.
Mazishi ya Silvanus Makalu
Ngofilo yatafanyika kesho Jumapili kijijini kwao Mwamanyili, Wilayani ya
Busega mkoa wa Shinyanga ambapo TFF itawakilishwa na Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji, Vedasto Lufano.
Marehemu Ngofilo wakati wa uhai
wake aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa FAT wakati wa Muhidin Ndolanga na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya FAT, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa
Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA) 1984-1994, ambapo baada ya kustaafu alipewa
wenyekiti wa heshima na MZFA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni