SERIKALI KUPUNGUZA VIZUIZI KWA MAGARI YANAYOKWENDA NJE YA NCHI.SERIKALI KUPUNGUZA VIZUIZI KWA MAGARI YANAYOKWENDA NJE YA NCHI.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, 
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph Nyamhanga 
ametambulisha utaratibu mpya utakaotumika kupunguza vikwazo visivyo vya 
kiforodha ili kurahisisha biashara na usafirishaji kwa magari makubwa 
yanayosafiri kwenda nje ya nchi.
Utaratibu huo unaotarajiwa kuanza
 Mei mwaka huu utawezesha magari yanayosafiri nje ya nchi kukagulia 
katika vituo visivyozidi vinne ili kupunguza muda wa safari kwa magari 
yaendayo nje ya nchi na kuvutia wasafirishaji kutumia bandari ya Dar es 
Salaam.
“Tumetayarisha stika 
zitakazobandikwa kwenye magari yanayokwenda nje ya nchi ambayo 
yatasimama na kukaguliwa katika vituo vitatu kwa magari yanayotumia 
barabara ya kanda ya kati na vinne kwa yanayotumia kanda ya Dar es 
salaam yaani TANZAM ”amesema Eng. Nyamhanga.
Eng. Nyamhanga amevitaja vituo 
hivyo vya barabara ya ukanda wa kati kuwa ni Vigwaza mkoani Pwani, 
Manyoni mkoani Singida na Nyakanazi mkoani Kagera na kwa ukanda wa Dar 
es salaam yaani barabara kuu ya TANZAM- Dar es salaam hadi Tunduma na 
Uyole hadi Kasumulu vitatumika vituo vine ambavyo ni Vigwaza mkoani 
Pwani,Mikumi mkoani Morogoro,  Makambako mkoani Njombe na Mpemba mkoani 
Songwe.
Vituo hivyo vya ukaguzi wa pamoja
 vitakuwa na huduma ya Mizani, Vituo vya Polisi, Mamalaka ya Mapato 
Tanzania (TRA), na maeneo ya kupumzikia madereva wanaosafiri kwenda nje 
ya nchi.
Katika hatua nyingine Eng. 
Nyamhanga amesema ili kurahisisha biashara ya usafirishaji kati ya 
Tanzania na Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya 
Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC), na Jumuiya ya Soko la Pamoja kwa 
Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) Serikali inaendelea 
kutoa huduma za pamoja mipakani one stop border post 
inayolenga kurahisisha huduma za forodha,uhamiaji na usimamizi wa ubora 
wa bidhaa na huduma ,ulinzi na usalama kwa kutoa huduma hizo upande 
mmoja wa mpaka kwa nchi mbili husika.
Vituo hivyo vinavyojengwa katika 
mipaka ya Holili, Namanga, Horohoro,Sirari, Mtukula, Rusumo, Kabanga, 
Tunduma na Kasumulu vitaimarisha huduma za forodha,uhamiaji ulinzi na 
usalama.
Imetolewa na Kitengo cha habari na mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi).
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni