By Raymond Urio, Dar
UMOJA wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania umefunguliwa rasmi leo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi, Sophia Mjema, kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam leo, kwa mwaka 2016,2017 chini ya Udhamini wa Kampuni ya Coca Cola ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo kila mwaka nchini.
Akizungumza katika Uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Nchini Bi, Sophia Mjema alisema kuwa Serikali inaishukuru Kampuni hiyo kwa msaada wanao utoa kwa lengo la kuinua vipaji nchini, alisema Sophia Mjema.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Vinywaji Baridi Coca Cola, Njowoka Maurice Lengo Kuu la Mashindano hayo ni Kuinua vipaji kwa vijana walioko kwenye Shule za Sekondari nchini ambapo mwisho wa siku ni kuja kupata wachezaji na wasidizi wazuri kwenye Taifa letu kwa Upande wa Michezo alisema , Njowoka.
Mkuu wa Wilaya akiongean na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania ( BMT), Mohammed Kiganja kwenye ofiisi za Uwanja huo leo jijini, Dar es Salaam. Picha zote na Raymond Urio
Baadhi ya Wanafunzi na wageni wakiwa kwenye jukwaa kwenye Ufunguzi huo wa UMISETA, kwa Mkoa wa Dar es Salaam leo.
Meneja Biashara ya Kampuni ya Coca Cola, Njowoka Maurice ( Kulia), akibadilishana wazo na mmoja wa wafanya kazi wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Shule ya Makongo High wakiwa uwanjani Teyari kwaajili ya Ufunguzi wa Mashindano hayo.
Wachezaji wa Shule ya Sekondari Trilav, wakiwa uwanjani kwaajili ya kujiandaa na mechi ya Ufunguzi wa Mashindano hayo.
Mkuu wa wilaya akitoa vifaa vya Michezo kwa Wanafunzi wa Sekondari ya Magereza na Azania leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi, Sophia Mjema akikagua vikosi vyote vya timu kwenye ufunguzi huo leo.
Akitoa neno kwa wachezaji wa timu zote kwenye Ufunguzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Temeke na Mgeni rasmi Sophia Mjema akizindua Mashindano hayo leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu ya Mpira wa Kikapu ya Shule ya Makongo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni