Benki ya Exim yazindua mashine yake ya kwanza ya kuweka pesa kwenye akaunti.Benki ya Exim yazindua mashine yake ya kwanza ya kuweka pesa kwenye akaunti.
……………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
BENKI ya Exim Tanzania imezindua 
mashine yake ya kwanza ya kuweka pesa (CDM) itakayowawezesha wateja wa 
kampuni ya Pacific International Lines, PIL kuweka pesa kwenye akaunti 
zao moja kwa moja bila kulazimika kufika kwenye ofisi au kuhudumiwa na 
wafanyakazi wa benki hiyo.
Ufunguzi wa mashine hiyo 
ulifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni ukihusisha mwakilishi wa 
benki hiyo ambaye ni Mkuu wa  Huduma za matawi Bw Eugine Massawe pamoja 
na Meneja Mkuu wa kampuni ya PIL Bw. Kevin Stone.
Akizungumzia mashine hiyo iliyopo
 kwenye jengo la Maktaba (Makataba Square)lililopo katikati ya jiji, Bw 
Massawe alisema ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika 
kurahisisha huduma zaidi za kifedha kwa wateja wa benki hiyo.
“Mashine hii itawawezesha wateja 
wetu kuweka pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao wao wenyewe. Huduma 
hii itapatikana kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 na nusu jioni kila 
siku na itatoa fursa kwa wateja         wa PIL kupata msaada kutoka kwa 
wahudumu wetu waliopo jirani na mashine pale watakapohitaji,’’ alisema
Kwa mujibu wa Bw Massawe, kwa 
kuanzia mashine hiyo itaanza kupokea noti za Dola ya Kimarekani kwa 
kiasi chochote huku akitahadharisha; “Ifahamike kwamba mashine hii ina 
uwezo mkubwa wa kutambua pesa bandia au zile zisizofaa kwa kuwa 
imewekewa mfumo bora kabisa wa kiusalama,”
Aliongeza kuwa mashine hiyo 
inamuwezesha mtumiaji  kupata risiti ya muhamala atakaoufanya sambamba 
na kumuhakikishia mafanikio ya muhamala husika.
“Mteja atapokea ujumbe mfupi wa 
maneno kuhusiana na mwenendo ya muhamala alioufanya,’’ alisema Bw 
Massawe huku akisisitiza: “Benki ya Exim itabaki kuwa benki pekee yenye 
kubuni huduma zinazokidhi matakwa ya wateja kulingana na mabadiliko ya 
kimahitaji katika huduma za kibenki,’’
Alisema huduma hiyo imewekwa 
jirani na makao makuu ya benki hiyo ili kuwawezesha watumiaji wa huduma 
hiyo kupata msaada kwa urahisi kutoka kwa wafanyakazi wa benki pale 
wanapohitaji.
“Itakapofikia kipindi ambacho 
wateja wetu watakuwa tayari wamejenga uelewa wa kutosha kuhusiana na 
matumizi sahihi ya mashine hii tutakuwa tayari kuongeza mashine nyingine
 katika maeneo mbalimbali ili waweze kufurahia huduma hii zaidi,’’ 
aliahidi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni