CHAMA CHA UDP CHAPATA PIGO VIGOGO WAKE WAWILI WAKIMBILIA CCK
 Katibu
 Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza
 na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akiwapokea waliokuwa 
viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama
 chama ambao ni  Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa 
Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi  Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na 
Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa 
Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa
 katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi 
mbele ya waandishi wa habari.
 Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK. 
 Katibu
 Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi 
kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam, 
Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa 
chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu
 Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi 
kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum 
Makunganya aliyehamia chama hicho.
…………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
CHAMA
 cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa 
Taifa, John Momose Cheyo, kimepata pigo baada ya wenyeviti wawili wa 
mikoa ya Mtwara na Dar es 
Salaam kukihama na kujiunga na Chama Cha Kijamii (CCK).
Viongozi waliokihama chama hicho ni  Salum Makunganya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara,  Mkurugenzi wa Uchaguzi  Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho na
 Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmshauri Kuu, 
Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga 
CCK leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa 
habari.
Wenyeviti
 hao baada ya kujitoa walikabidhi kadi zao za UDP kwa Katibu Mkuu wa 
CCK, Renatus Muabhi ambaye naye aliwakabidi kadi ya CCK na kuwatangaza 
rasmi  kuwa wanachama wa chama hicho.
Makunganya
 alikabidi kadi yake ya UDP yenye namba 4544 na kukabidhiwa ya CCK namba
 1597 huku Mwakitiga akibidhi kadi yake ya UDP namba 2852 na kukabidhi 
ya CCK yenye namba 01599 katika tukio lililofanyika ofisi za CCK.
Wakizungumzia
 sababu zilizowafanya wajitoe UDP walisema ni kutokana na chama hicho 
kutokuwa na mwelekeo wa kimaendeleo ambacho kwa zaidi ya miaka sita 
viongozi wake wa kitaifa hawajaitisha mikutano ukiwamo wa Halmashauri 
Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.
Walisema
 sababu nyingine ni kwamba viongozi wa kitaifa wa UDP wamekigeuza chama 
hicho kama kampuni binafsi ambapo wamekuwa wakitoa maamuzi mbalimbali 
ambayo hayajaamuliwa na wanachama kwenye vikao .
“Nyie
 waandishi si mnaishi Dar es Salaam tangu lini mlishaona Mwenyekiti wa 
Taifa wa UDP, John Cheyo akiitisha hata mkutano wa hadhara hapa Dar es 
Salaam kuzungumzia mambo mbalimbali ya chama na taifa kwa ujumla kama 
vinavyofanya vyama vingine…jibu ni hakuna, UDP inabuka tu wakati wa 
uchaguzi na tena kwenye eneo moja tu,”alisema Mwakitiga.
Muabhi
 akizungumza baadhi baada ya kuwakabidhi kadi wenyeviti hao alisema CCK 
inawapokea kwa mikono miwili viongozi hao na kwamba wakiwa ndani ya 
chama hicho wataona utofauti na vyama vingine kwa kuwa chama kimejiwekea
 misingi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Muabhi
 aliitaka serikali kulitazama upya suala la vikao vya Bunge kutotangazwa
 kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo kunawanyima haki 
wananchi ya kupata habari na hivyo kushindwa kujua nini kinaendelea 
Bungeni.
“Serikali
 ijitathimini, wananchi wasipojua nini kinaendelea Bungeni kuna haja 
gani kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenda Bungeni, 
wananchi watajuaje kama wawakilishi wao wamezifikisha kero zao 
serikalini,”alisema.
Mwenyekiti
 wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma, alisema ujio wa wanachama hao wapya
 ambao ni wakongwe katika siasa na hivyo CCK itajifunza mambo mengi 
kutoka kwao.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni