DC HAPI ATEMBELEA WANANCHI WA BUNJU, MBWENI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO
Mkuu
 wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo 
amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero 
mbalimbali.
Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mkuu wa Wilaya akiambatana na Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam na mainjinia wa manispaa alitembelea eneo hilo na kuona adha inayowapata wananchi.
Akipokea maelezo ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa na baadae kuzungumza na wananchi wa eneo hilo, mkuu wa wilaya aliambiwa na baadhi ya wakazi wa asili wa eneo hilo kuwa sehemu hiyo ilikua ni bwawa la maji miaka yote.
Wakazi hao ambao nyumba zao zimezungukwa na maji walimuomba Mkuu wa wilaya kusaidiwa pampu kubwa ili maji hayo yavutwe na kupelekwa kwenye mitaro upande wa pili wa barabara.

Akijibu maombi hayo Mh. Hapi 
aliwaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa
 kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo. Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ya 
Kinondoni aliwaambia wananchi kuwa wale wote waliojenga  katika eneo 
hilo ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo la wazi wajiandae kuondoka.
“Serikali itawasaidia kutoa haya 
maji kama hatua ya dharura. Lakini suluhu ya kudumu ni kuwa waliojenga 
hapa wote wamejenga eneo la wazi tena ni bwawa. Hivyo lazima wajiandae 
kuhama.
Serikali kazi yake ni kuwaambia wananchi ukweli, hata kama ukweli huo utakua na maumivu. Hivyo ukweli wa jambo hili ni kuwa waliojenga hapa wahame.”
Serikali kazi yake ni kuwaambia wananchi ukweli, hata kama ukweli huo utakua na maumivu. Hivyo ukweli wa jambo hili ni kuwa waliojenga hapa wahame.”
Akitoa rai kwa viongozi wa 
serikali ya mtaa ambao wameshiriki katika kuuza eneo hilo kinyume na 
taratibu mh. Mkuu wa Wilaya aliagiza na kusema
” kila Mwananchi aliyejenga hapa 
aende ofisi ya mtaa kujisajili akiwa na vielelezo vyote vya kumiliki 
eneo hili na alikonunua. Kisha nipewe taarifa na uhakiki utafanyika. 
Kama kuna viongozi wa serikali ya mtaa walishiriki kuuzia watu viwanja 
hapa kinyume na ramani ambayo wao wana nakala yao basi wajiandae 
kuwajibishwa.”
Katika hatua nyingine Mkuu wa 
Wilaya alitembelea eneo la Mbweni ambako Mwananchi asiyefahamika 
amejenga ukuta kuzunguka eneo la wazi. Hapi alifika eneo hilo na 
kujionea ukuta huo kisha akaagiza mtendaji wa mtaa pamoja na anayejenga 
ukuta huo kufika ofisini kwake kesho Ijumaa mchana wakiwa na vielelezo 
vyote na vibali vya ujenzi kama wanavyo.
Ziara ya mkuu wa wilaya inaendelea muda huu katika maeneo ya barabara za Sinza ambazo wakandarasi walipewa kujenga
Ziara ya mkuu wa wilaya inaendelea muda huu katika maeneo ya barabara za Sinza ambazo wakandarasi walipewa kujenga
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni