WANAMTANDAO WAITAKA DAWASCO KUTUPIA JICHO TABAKA LA WASIOJIWEZAWANAMTANDAO WAITAKA DAWASCO KUTUPIA JICHO TABAKA LA WASIOJIWEZA
Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam
(DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo na ujumbe kutoka
Mtandao Kijinsia Tanzania (TGNP) walipofika ofsini hapo kwa ajili ya
kutoa shukrani zao.
…………………………………………………………………………………………
WANAMTANDAO WAITAKA DAWASCO KUTUPIA JICHO TABAKA LA WASIOJIWEZA
WANAHARAKATI
WA Mtandao wa kijinsia “TGNP” wamepongeza juhudi zinazofanywa na
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), kutokana na
Mabadiliko na jitihada zinazofanywa na Dawasco za kuboresha huduma ya
Maji pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii inayoizunguka.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja na Dawasco, Mratibu wa kampeni ya Maji ya “MAMA
TUA NDOO KICHWANI” kutoka Mtandao wa Kijinsia Bi. Martha Samwel.
Ameitaka
Dawasco kuhakikisha inapeleka huduma ya Majisafi na salama katika
sehemu zote muhimu ikiwamo mashuleni na hospitalini ili kumpunguzia
mwanamke adha ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu pamoja na kumuondolea
mwanamke adha ya kubakwa na hata kupigwa kutokana na kuhangaika
kutafuta Maji.
“Tunataka
kutoa salamu za pongezi kwa DAWASCO kwa mabadiliko na jitihada
tunazoziona za kuboresha huduma ya Maji na kufanya kazi ya kusaidia
jamii, tumefurahishwa na jitihada zenu, tutafanya kazi pamoja ili
kuhakikisha tunamuondolea mwanamke shida ya kupoteza muda mwingi
kuhangaika kutafuta Maji kwani kampeni yenu ya “MAMA TUA NDOO YA MAJI
KICHWANI” ndio kampeni yetu” alisema Bi. Martha.
Aidha,
Mwanaharakati wa mtandao wa kijinsia Bi. Gema Akilimali, amefurahishwa
ya kampeni ya Mama tua ndoo kichwani kwani itamsaidia mwanamke kwa kiasi
kikubwa kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi, kitendo
ambacho kwa sasa hatimizi ipasavyo kutokana na kutumia muda mwingi
kutafuta maji, pia anaamini utaongeza ufaulu mashuleni kwani badala ya
watoto wa kike kutumia muda mwingi kutafuta Maji sasa wataweza kuokoa
muda na kuwa kushiriki masomo ipasavyo.
“Wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta Maji, hivi ni saa ngapi ataleta maendeleo ya nchi? Lazima tumkwamue mama katika janga
hili ili na yeye aweze kujenga nchi yake” alisema Bi. Akilimali.
hili ili na yeye aweze kujenga nchi yake” alisema Bi. Akilimali.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja,
amehaidi hadi kufikia Disemba 31 watahakikisha kampeni ya mama tua ndoo
ya Maji kichwani itawafikia wakazi wengi wa Dar hususani wale walio
katika tabaka la chini.
Aidha
amehaidi kutoa huduma ya Majisafi na salama bure kwa wazee, walemavu na
yatima wote ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za kuunganisha huduma
ya Maji, pamoja na kujenga pointi za ya kunywea Maji katika sehemu
mbalimbali za Jiji ikiwa nipamoja na maeneo ya stendi ya Mabasi ya
Ubungo, Buguruni chama, Magomeni Mapipa na Kisutu stendi ya zamani.
“Mimi
pamoja na menejimenti yangu tunaenda kumtua mama ndoo ya Maji kichwani
mpaka kufikia mwishoni wa mwaka huu, kwani Maji yatakuwa mengi katika
maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam pamoja na Pwani” alimalizia
Mhandisi Luhemeja
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni