BARAZA LA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA UJENZI LAKUTANA
Mwenyekiti
wa Baraza la Wafanyakazi Sekta ya Ujenzi ambaye ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph
Nyamhanga, akiongea na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi sekta ya ujenzi
kabla ya kulifungua rasmi baraza hilo lililofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mtafiti
wa masuala ya Hifadhi ya Jamii kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bw. Michael Semiono akifafanua jambo kwa
wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi.
Baadhi
ya Watendaji Wakuu wa Sekta ya Ujenzi wakiwa katika kikao cha Baraza la
Wafanyakazi sekta ya ujenzi lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi (sekta ya ujenzi)
wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi
Sekta ya Ujenzi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano wa sekta hiyo Eng. Joseph Nyamhanga, katika kikao cha Baraza
la Wafanyakazi kililofanyika jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni