WAKANDARASI WAPIGA MARUFUKU MAGARI YENYE UZITO MKUBWA KUPITA DARAJA LA NYERERE,WAWATAKA WATANZANIA KULITUNZA DARAJA HILO.
Hivi
 ndivyo mandhari nzuri na ya kuvutia ya Daraja la Nyerere lionekanavyo 
kwa juu pamoja na flai ova yetu ya kuingilia darajani hapo ndani ya 
Wilaya mpya ya Kigamboni.
Sehemu ya mageti ambapo magari yanapaswa kupita wakati wa kufanya malipo yanayotarajiwa kuanza Mei Mosi 2016.
Mhandisi
 wa Mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group
 and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) Jamal Mruma akitoa ufafanuzi 
kwa Wanahabari kuhusiana na ubora wa daraja hilo.Mhandisi Mruma alisema 
kuwa Daraja hilo limejengwa kwa ubora mkubwa na lina uwezo wa kuhimili 
uzito zaidi ya tani 50,lakini kwa sasa magari yanayoruhusiwa ni yale 
yenye tani kumi kushuka chini,”kwa sasa tunadhibiti uzito mkubwa kwa 
sababu kuna baadhi ya maeneo bado hayajakamilika ikiwemo na barabara ya 
kuingilia Kigamboni,ambako hakuwezi kumudu kupitishwa uzito 
mkubwa”,alibainisha Mhandisi Jamal.
Meneja
 Mradi kutoka NSSF,Mhandisi Karim Mataka akizungumzia namna baadhi ya 
Madereva ambao wamekuwa wakikiuka taratibu/sheria na alama zilizowekwa 
katika daraja hilo kubwa Afrika Mashariki ambalo linatarajiwa kudumu kwa
 zaidi ya miaka 100 iwapo litapata matunzo stahiki.Mhandisi Karimu 
amebainisha kuwa magari yanayopaswa kupita hapo kwa sasa yawe chini ya 
tani 10,kwa sababu kwa upande wa Kigamboni bado baadhi ya barabara 
hazijakamili,hivyo ni vyema Madereva wote wakawa makini.
Daraja
 hilo ambalo litaanza kutumika rasmi kwa kulipia Mei Mosi 2016,Mhandisi 
Karimu amewataka Watanzania kulinda miundo mbinu ya daraja hilo ikiwemo 
kutii sheria zote za Daraja hilo ili kuepuka kusababisha uharibifu wa 
aina yoyote ile,kwa sababu limejengwa kwa gharama kubwa na linahitaji 
matunzo.
Mhandisi
 alibainisha pia kuwa Daraja hilo la Kigamboni ambalo lilizinduliwa na 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na 
kulibatiza jina la Daraja la Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Serikali
 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii 
(NSSF),
Moja ya Lori likikatiza darajani hapo kwa kukiuka taratibu na sheria za Daraja hilo.
Muonekano
 wa Daraja la Mwal Nyerere kama lionekanavyo kwa mbaali kidogo 
unapoelekea kwenye mageti ya kutokea upande wa pili wa Kigamboni.Daraja 
hilo limerahisisha usafiri wa kutoka Kigamboni mpaka kati kati ya jiji 
la Dar.
 





 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni