Juliana Shonza asema amejipanga vilivyo kuwakwamua wanawake kiuchumi mkoani Songwe
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa 
Songwe, Juliana Shonza, akiwa amebebwa na Wanawake, Wajumbe wa Baraza la
 Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Momba mkoani hapa jana 
alipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua 
katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Picha na Mpigapicha Wetu
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa 
Songwe, Juliana Shonza, akizungumza na wanawake, Wajumbe wa Baraza la 
Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe, 
jana alipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru kwa 
kumchagua kwake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Picha na Mpigapicha 
Wetu
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa 
Iringa, Rose Tweve (kulia)  akimsisitiza jambo Mbunge mwenzie wa Mkoa wa
 Songwe, Juliana Shonza jana wakati Shonza alipokutana na Wajumbe wa 
Baraza la Wanawake wa CCM (UWT)  Wilaya ya Momba   mjini Tunduma kwa 
lengo la kuwashukuru wajumbe hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa viti 
maalum mkoani hapa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Picha na 
Mpigapicha Wetu.
Mbunge wa  Viti Maalum, Mkoa wa 
Songwe, Juliana Sonza na Mbunge mwenzia wa Mkoa wa Iringa, Rose  Tweve (
 wa tatu kushoto) wakiserebuka na wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CCM 
Wilaya ya Momba (UWT)  Mkoa wa Songwe, jana walipokutana nao mjini 
Tunduma kwa lengo la kuwashukuru  kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa 
mwaka jana kupitia UWT. Picha na Mpigapicha Wetu.
…………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Tunduma. Mbunge wa Viti Maalumu 
Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza amesema amejipanga vilivyo kuhakikisha 
anawainua wanawake wa mkoa  huo, kiuchumi kwa kuwazesha kufanya 
ujasiriamali utakaowaingizia kipato.
Shonza alitoa kauli hiyo jana 
 kwa  wajumbe wa Baraza la Wawanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) 
Wilaya ya Momba, alipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru 
kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Shonza ambaye aliongozana na 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve, alisema  katika 
kuhakikisha adhima yake  ya kuwanua wanawake hao inatimia ameanzisha 
mfuko maalumu alioita ‘Songwe Women Foundation”   utakaolenga kuwasaidia
 wanawake wa umoja huo.
“Ninawaombeni sana undeni 
vikundi, hakikisheni mnavisajili na fedha ya kusajili vikundi vyenu 
nitatoa mimi, na nimeanzia mfuko maalum kwa ajili ya wanawake wote wa 
mkoa wa Songwe, na nimeweka Sh 20 milioni na kila kikundi kwenye kata 
zenu mtapewa Sh200,000 kwa ajili ya kuanzisha  mradi mtakaona unafaa. 
Niliwaahidi kuwainua nitafanye mtakavyotaka nyinyi.
Kupitia mfuko huo, nitataka 
mniambie ni mradi gani mnataka kuufanya. Lakini mbali na kuwawezesha 
kifedha lakini kabla ya kuanza kuanzisha mradi huo kwanza nitawaletea 
wataalamu wa masomo ya ujasiriamali watawafundisha ili iwasaidie 
kuendesha mradi wenu,” alisema Shonza.
Alisema kupitia mfuko huo, tayari
 ameanza kuzungumza na wadau mbalimbali watakaomsadia kuwawezesha 
wanawake wa mkoa wake kujikwamua kiuchumi huku akiwasisitizia kuchapa 
kazi bila kuchoka wala kubweteka kwa vile wanapata msaada kutoka kwake.
Kwa upande wake, Mbunge wa 
Iringa, Tweve aliyemsindikiza Shonza kuzungumza na wanawake hao, 
aliwataka wanawake wa Songwe kujivunia mbunge wao (Shonza) kwani ni 
mchapa kazi na ni mtu mwenye mtandao npana ambao utawawezesha 
 kujikwamua kiuchumi.
“kwanza ninawashukuru sana 
wanawake wa Momba, na Songwe kwa ujumla kumuamini motto wenu huyu 
Shonza, ni muda mfupi nimefahamiana naye. Na hii ni kutokana na uchapa 
kazi wake, ninaombe mtumieni vyema bila kusahau na nyinyi kufanya kazi 
bila kuchoka.” Alisema Tweve.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya 
Momba, Isavera Mwanisenga alisema CCM katika uchaguzi uliopita 
walipoteza majimbo yote mawili ya Momba na Tunduma hivyo lakini bado 
hawajafa moyo kwani bado wanaye mbunge Shonza anawapigania huku 
wakiendelea kujipanga kurudisha majimbo hayo kwenye uchaguzi mkuu wa 
mwaka 2020.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni