TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MNAMO TAREHE 18.04.2016 MAJIRA YA 
SAA 03:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MALAMBO, KATA YA RUIWA, TARAFA YA
 ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WATU WANAOSADIKIWA KUWA 
MAJAMBAZI AMBAO IDADI YAO HAIKUWEZA KUFAHAMIKA MARA MOJA WALIFIKA 
NYUMBANI KWA GERVAS LAZARO [56] MFANYABIASHARA NA MKE WAKE AITWAE 
WITNESS MWAKALENGA [50] WOTE WAKAZI WA MALAMBO KWA LENGO LA KUFANYA 
UHALIFU WA KUJARIBU KUNYANG’ANYA KWA KUTUMIA SILAHA.
HATA HIVYO KUTOKANA NA KUWEPO KWA 
TAARIFA ZA SIRI KUHUSIANA NA NJAMA NA MPANGO HUO, ASKARI POLISI WALIKUWA
 TAYARI ENEO HILO LA TUKIO ILI KUWEZA KUKABILIANA NA MAJAMBAZI HAO.
KATIKA KUKABILIANA NA MAJAMBAZI 
HAO, BAADHI YA ASKARI WALIIMARISHA ULINZI ENEO HILO NA KUFANIKIWA KUPATA
 PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.913 CGF AINA YA T-BETTER RANGI 
NYEKUNDU AMBAYO ILIKUWA IKITUMIWA NA MAJAMBAZI HAO. BAADA YA UCHUNGUZI 
PIKIPIKI HIYO ILIBAINIKA KUWA NA INJINI NAMBA ZJ16ZFNJC2512944 NA 
CHASSES  LZEPCKLASCL812905 AMBAYO ILITELEKEZWA NA MAJAMBAZI HAO BAADA YA
 KUONA POLISI WAMEDHIBITI ENEO HILO.
HATA HIVYO POLISI KWA KUSHIRIKIANA
 NA WANANCHI WA ENEO HILO WALIENDELEA KUWAFUATILIA MAJAMBAZI HAO NA 
KUFANIKIWA KUPATA SILAHA MOJA AINA YA SMG NAMBA UA 2911997 PAMOJA NA 
RISASI 27 KWENYE MAGAZINE. AIDHA KATIKA ENEO HILO LA TUKIO AMBALO 
ILIKUTWA SILAHA HIYO PIA ILIKUTWA KOFIA MOJA YA KUFICHA SURA [MZURA] 
ILIYOTELEKEZWA NA MAJAMBAZI HAO KABLA YA KUKIMBILIA PORINI.
KWA SASA MSAKO /DORIA INAENDELEA 
MAENEO YA PORI LA NARCO LILILOPO KATI YA WILAYA YA MBARALI NA CHUNYA, 
AMBAPO KIKOSI KAZI CHA ASKARI WA WILAYA HIZO WAMEUNGANA ILI KUWASAKA 
MAJAMBAZI HAO KWA AJILI YA KUWAKAMATA. AIDHA TARATIBU ZIMEFANYWA ZA 
KUSHIRIKISHA VIONGOZI WA VIJIJI VILIVYOPO MAENEO JIRANI NA MSITU HUO ILI
 KUSAIDIANA KUWAPATA MAJAMBAZI HAO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.341 
BYR IKIWA NA TELA YENYE T.557 BEP AINA YA BEIBEN- TANKER IKIENDESHWA NA 
DEREVA AITWAYE OSWINI NUNGU [43] MKAZI WA JIJINI DSM IKIWA IMEBEBA 
SHEHENA YA MAFUTA AINA YA DIESEL IKITOKEA DSM KUELEKEA NCHINI ZAMBIA 
ILITEKETEA KWA KUUNGUA MOTO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 
21.04.2016 MAJIRA YA SAA 15:15 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MALENGA, 
KATA YA MBUYUNI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA CHANZO CHA AJALI HIYO NI 
HITILAFU KATIKA MFUMO WA BREAK WA GARI HILO NA KUPELEKEA GARI KUUNGUA 
MOTO. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. THAMANI YA 
UHARIBIFU BADO KUFAHAMIKA. UPELELEZI UNAENDELEA.
            Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni