Mh. Rugimbana aipongeza timu ya Uchukuzi SC
Mgeni
 rasmi Afisa Maendeleo Vijana,, Tumsifu Mwasambale akitoa hotuba alipo 
mwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mh. Jordan Rugimbana.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Mei Mosi, Joyce Benjamin akitoa hutoba yake.
 Bendi ya Watoto wa shule ya msingi ya St. Tom wakiongoza maandamano ya 
timu shiriki za mashindano ya Mei Mosi kuingia uwanjani. 
Timu
 ya Uchukuzi SC wakiwa wamejipanga uwanjani wakimsikiliza mgeni rasmi, 
Afisa Maendeleo Vijana, Tumsifu Mwasambale (hayupo pichani).
………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MKUU wa mkoa wa Dodoma, Jordan 
Rugimbana ameipongeza timu ya Uchukuzi SC kwa kuleta wachezaji wengi 
kwenye mashindano ya Mei Mosi yaliyoanza Aprili 18 mwaka huu kwenye 
uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mh. Rugimbana katika hotuba ya 
ufunguzi wa mashindano hayo iliyosomwa jana na Afisa Maendeleo Vijana wa
 ofisi ya mkuu wa mkoa, Tumsifu Mwasambale kwa niaba yake, alisema kuwa 
amedokezwa na waandaaji kuwa Uchukuzi SC ndio timu pekee iliyoweza 
kuleta wachezaji wengi, hivyo anawapongeza viongozi wao.
“Ninaipongeza Uchukuzi SC pamoja 
na kudokezwa pia nimeona kwa macho yangu wakati wa maandamano ya timu 
zikiingia uwanjani  kuwa Uchukuzi SC ndio wenye wachezaji wengi zaidi, 
nawapongeza sana viongozi wao, wanatambua umuhimu wa michezo mahala pa 
kazi,” alisema.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa timu 
ya Uchukuzi SC, Alex Temba amesema timu yake imekuja na wachezaji 
takribani 96 ambao watashiriki kwenye michezo ya kuvuta kamba, netiboli,
 riadha, kuendesha baiskeli, soka, bao, karata na darts.
Tayari timu hiyo inayoundwa na 
wachezaji kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Bandari (TPA), Anga
 (TCAA), Hali ya Hewa (TMA) na Chuo cha Bandari (DMI),  imeshinda kwenye
 mechi zake za soka dhidi ya Ukaguzi magoli 3-1 na upande wa netiboli 
waliwafunga CDA magoli 23-15.
Hatahivyo, Mh. Rugimbana 
aliwashutumu na kusema sababu zilizotolewa na viongozi hao kuzuia timu 
zao kushiriki kwenye mashindano ya mwaka huu kwa kisingizio cha Mh. Rais
 John Magufuli kuzuia michezo hii, hazina mashiko na ni kisingizio 
kilichopaswa kukemewa vikali.
Alisema hajawahi  kumsikia Mh. 
Rais Magufuli akizuia michezo ya Mei Mosi, na mingine yeyote bali 
walimsikia akitoa maelekezo ya kuzuia sherehe za Uhuru na sasa Muungano,
 na kutoa maelekezo na tayari yanmefatwa kwa ufanisi mkubwa na wahusika.
“Ni uoga usiokuwa na mashiko, 
kwani hata ingekuwa Mh Rais kazuia michezo,  hata Mh. Waziri Mkuu 
(Kassim Majaliwa) asingekuwa na nguvy ya kukutana na viongozi wa 
mashirikisho na vyama vya michezo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, 
takribani miezi mitatu iliyopita wakijadili uimarishaji wa michezo, na 
walaumu sana viongozi  waliowanyima haki wanamichezo kushiriki kwenye 
michezo hii,” alisema Rugimbana.
Mashindano ya mwaka huu yenye 
kauli mbiu ya hapa kazi tu isiwe kisingizio kwa waajiri kuondoa michezo 
kazini, yamekuwa na idadi ndogo ya washiriki, ambapo hadi jana ni timu 
14 pekee ndizo zilizofika Dodoma.
Hatahivyo, awali Kaimu Makamu 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mei Mosi, Joyce Benjamin, naye katika hotuba ya 
ufunguzi aliwalaumu viongozi kuzuia timu zao kwa kumsingizia Mh. Rais 
kuwa amezuia michezo.
 “Kumbukeni Mh. Rais wetu ni mmoja
 wa wanamichezo na ndio maana hata wakati wa kampeni tulimuona wote 
akipiga pushapu jukwaani, sasa iweje leo hii viongozi wa sehemu za kazi 
waseme amekataza michezo, michezo huu ni mikubwa imepata Baraka zote 
kutoka TUCTA (Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi) na Baraza la Mic
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni