DR. SHEIN KUONGOZA KAMATI MAALUM YA NEC ZANZIBAR
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati
Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mama Waride Bakari
Jabu imesema kikao hicho kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, iliyopo mtaa wa
Kisiwandui, Mjini Unguja.
Taarifa
imesema kikao hicho kawaida cha siku moja, pamoja na mambo mengine
kitapokea na kujadili taarifa kadhaa kutoka Idara na Vitengo mbali mbali
vya Chama hicho, ikiwemo taarifa ya hali ya kisiasa ya Zanzibar, kabla
na baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar.
Kikao
hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC
Zanzibar, kilichofanyika April 20, mwaka huu, chini ya M/kiti wake
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, kwa ajili ya
kuandaa ajenda za kikao hicho.
Taarifa
imesema kikao hicho kinafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 114 (b) ya
Katiba ya CCM, Toleo la mwaka 2012 na kwamba maandalizi yote
yamekamilika.
Sgd.
(Waride B. Jabu),
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
Idara ya Itikadi na Uenezi – CCM,
ZANZIBAR. 22/04/2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni