NHIF YAPELEKA HUDUMA YA MADAKTARI BINGWA MKOANI NJOMBE
Mganga Mkuu wa  mkoa wa Njombe 
Dokta Samuel Mgema akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma  za 
madaktari bingwa mjini Njombe wanaowafanyia upasuaji na matibabu 
 wagonjwa mbalimbali kwa  mikoa husika, kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali
 Profesa Mohammed Bakari
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na 
Ushauri wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dokta Frank Lekey akizungumza 
wakati wa uzinduzi wa huduma  za madaktari bingwa mjini 
Njombe wanaowafanyia upasuaji na matibabu  wagonjwa mbalimbali kwa 
 mikoa husika,kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed 
Bakari.
Baadhi ya watumishi na madaktari pamoja na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Mkuu wa mkoa wa NJOMBE  Mh. 
Rehema  Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja viongozi mbalimbali mara 
baada ya uzunduzi huo uliofanyika mjini Njombe leo.
………………………………………………………………………………………………..
Wizara ya Afya, Maendeleo ya 
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirkiana na Mfuko wa Taifa wa Bima
 ya Afya, wiki hii inaendesha zoezi la huduma za madaktari bingwa katika
 mikoa ya Njombe na Iringa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi 
wa zoezi hilo mkoani Njombe Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed 
Bakari amesema serikali itaendelea kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa 
Bima ya Afya kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapelekwa katika maeneo 
mengi ambako wananchi wanahitaji huduma za madaktari  bingwa ili 
kukabiliana na upungufu uliopo.
Amesema pamoja na kuendelea 
kutumia huduma hizo za muda za madaktari Bingwa, Serikali kupitia Wizara
 ya Afya, itajitahidi kujenga miundo mbinu bora ya sekta ya afya na 
kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi walio wengi.
Akizungumza kabla ya 
kumkaribisha Mganga Mkuu wa Serikali, Mganga Mkuu wa  mkoa wa Njombe 
Dokta Samuel Mgema, amesema hospitali yake inakabiliwa na changamoto 
nyingi ikiwa ni pamoja na uchakavu wa majengo na ufinyu wa nafasi 
ikilingwanishwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohudumiwa katika 
hospitali hiyo.
Ameomba Serikali iharakishe 
mchakato wa kujenga Hospitali mpya ya mkoa ili kukidhi mahitaji ya 
wananchi wa mkoa wa Njomba, kwani hospitali inayotumika hivi sasa ya 
Kibena ilikuwa na hadhi ya hospitali ya wilaya na kupandishwa hadi baada
 ya kutangazwa kwa mkoa mpya wa Njombe, miaka minne iliyipita.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za 
Tiba na Ushauri wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dokta Frank Lekey 
amesema huduma hizo za madaktari bingwa zimekuwa zikitolewa na Mfuko 
wake kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya kupeleka huduma 
bora za matibabu kwa wanachama wa NHIF na kwa wananchi kwa ujumla.
Asema hadi sasa huduma hizo 
zimeshatolewa katika mikoa 14, ambazo zaidi ya wagonjwa 11,400 
wamepatiwa huduma, miongoni mwao zaidi ya wagonjwa 340 walifanyiwa 
upasuaji wa kitaalamu.
Amesisitiza kuwa huduma hizo 
zinatolewa kwa wananchi wote bila ubaguzi kwa kufuata taratibu za 
kawaida za malipo za hospitali husika.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni