Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete na Mama Salma Kikwete wakaribishwa nyumbani kwa Mhe. Balozi Wilson M. MasilingiMheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete na Mama Salma Kikwete wakaribishwa nyumbani kwa Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi
Wiki
 iliyopita Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Washington, DC, alimkaribisha Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. 
Kikwete nyumbani kwake kwa chakula cha jioni na kujumuika pamoja na 
ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao walikuwa nchini 
Marekani kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya Benki ya Dunia (World Bank 
Group) na International Monetary Fund (IMF) tarehe 12 – 17 Aprili 2016. 
Kwenye ziara yake jijini Washington, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete 
alishiriki katika Kongamano la Kimataifa la Afya (World Health Congress)
 na Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kushauri Namna Bora ya 
Kugharamia Fursa ya Elimu kwa Wote Duniani (International Commission on 
Financing Global Education Opportunity).
Mhe.
 Rais  Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete katika
 picha ya pamoja na wenyeji wao, Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Mama 
Marystella Masilingi
Mhe.
 Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akibadiliashana mawazo na 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile 
(kushoto), Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Gavana wa Benki Kuu Prof. 
Benno Ndulu nyumbani kwa Mhe. Balozi , Tanzania House Bethesda, MD. 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni