UKWELI UKO WAPI KUHUSU KUSITISHWA KWA MATIBABU YA WAGONJWA WA SELIMUNDU (SICKE CELL) ?
By Raymond Urio, Dar
Yasmini Razack wanaharakati wa Ugonjwa wa Selimundu ( Sicke Cell ).
Kwa mujibu wa Muongozo wa Wizara ya Afya
Sikoseli inaingia katika orodha ya magonjwa yanayotakiwa kutibiwa bure,
na imekuwa ikifanyika hivyo lakini kuanzia tarehe 21 April mwaka huu,
kumekuwa na malalamiko kutoka kwa walezi wenye watoto wanaugua ugonjwa
wa Sikoseli kuwa wamekuwa wakitozwa pesa na matibabu ya ugonjwa huo
yamesitishwa katika hospitali ya Muhimbili.
Kufuatia hayo Mwanaharakati wa ugonjwa
wa Sikoseli Yasmini Razaak amelaani kitendo hicho alipokuwa anazungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuongeza kuwa
wagonjwa hao wameandikiwa barua na kupelekwa hospitali ambazo hazina
wataalamu wa ugonjwa huo ikwemo hospitali ya Amana na Temeke, hivyo
wamemuomba Rais Magufuli kuibeba agenda ya ugonjwa wa Sikoseli kama Rais
Kikwete alivyoibeba agenda ya ugonjwa wa Malaria na kuja na kampeni ya
Zinduka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Lawrence Msemu ( Kulia), akizungumza na waandishi kuhusiana na ufafanuzi wa matibabu ya wagonjwa wa Selimundu ( Sicke cell) wa habari jijini Dar es salaam jana . Picha zote na Raymond Urio
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Lawrance Msemu amekanusha kusitishwa
kwa huduma za matibabu na kutozwa pesa kwa wagonjwa wa sikoseli huku
akieleza kuwa kilicho sitishwa ni utafiti dhidi ya ugojwa huo hivyo
wananchi wataendelea na huduma hizo kama kawaida.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ameeleza kuwa hospitali yake imeamua
kufanya utaratibu kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa waliopo
hospitalini hapo (zaidi ya 6000), hivyo wagonjwa hao watapangiwa
hospitali zingine na endapo itashindikana kupata tiba stahiki watapewa
rufaa kwenda kwenye Hospitali hiyo ya Muhimbili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni