UCHAGUZI MKUU JUNI 05, 2016
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo
imetangaza Juni 05, 2016 kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi ndani ya
klabu ya Young Africans SC ya jijini Dar es salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili
Aloyce Komba amesema mchakato mzima wa uchaguzi wa klabu ya Young
Africans utakuwa ndani ya siku 33, ambapo mchakato unatarajiwa kuanza
rasmi Mei 03, 2016.
Komba
amesema jukumu lao Kamati ya Uchaguzi TFF ni kusimamia na kuhakikisha
Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo unafanyika katika hali ya demokrasia.
Ifuatayo ni kalenda ya mchakato wa Uchaguzi katika klabu ya Young Africans SC:
Mei
03, 2016 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, atatangaza mchakato wa
kulabu ya Young Africans, nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao
za matangazo.
Mei 04-9, 2016 – Kuanza kuchukua fomu za kugombea na mwisho wa kurudisha fomu kwa wagombea.
Mei
10, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itakaa kikao cha mchujo wa awali wa
wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa
awali.
Mei 11, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itachapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea.
Mei 12-13, 2016 Kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea wote.
Mei 14-15, 2016 Kamagi ya Uchaguzi TFF itapitia pingamizi zote na kufanya usajili wa wagombea.
Mei 16, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itatangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usahili.
Mei 17, 2016 Sekretarieti kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye Kamati ya Maadili ya TFF.
Mei 18-19, 2016 Kamati ya Maadili TFF itapokea, kusikiliza na kutolea maamuzi ya kamati ya maadili.
Mei 20, 2016 Kamati ya Maadili ya TFF itatangaza maamuzi ya kamati.
Mei 21-22, 2016 Kipindi cha kukata Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya Kimaadili kwenye kamati ya Rufaa ya Maadili TFF.
Mei 23, 2016 Kamati ya Maadili tff itasikiliza rufaa za kimaadili.
Mei 24, 2016 Kamati ya Rufaa ya Maadili itatoa maamuzi ya Rufaa.
Mei 25-26, 2016 Kipindi cha kukata Rufaa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi TFF.
Mei 27-28, 2016 Rufaa kusikilizwa na kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Mei 29, 2016 Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi TFF kutangaza maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Mei
30, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea
na kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo.
Mei 31 – Juni 04, Kipindi cha kampeni kwa wagombea.
Juni 05, 2016 siku ya Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Young Africans.
Wakati
huo huo Kamati ya Rufaa ya TFF Jumamosi, itasikiliza pia rufaa ya klabu
ya Geita Gold pamoja na rufaa ya kocha msaidizi wa Toto Africans Choke
Abeid,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni