BILA KUWEPO KWA YAYA TOURE NA RONALDO, MAN CITY, MADRID ZAMALIZA MCHEZO KWA SARE YA 0-0
Manchester City ikicheza bila ya kiungo wake wa "mipango" Yaya Toure, imeshindwa kuifunga Real Madrid katika mechi kali ya Ligi ya Mabingwa iliyochezwa kwenye Dimba la Etihad na kumalizika kwa sare ya 0-0.
Pamoja
na Madrid kumkosa Cristiano Ronaldo aliyekuwa jukwaani, lakini iliweza
kutawala zaidi na kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.
Mechi
hiyo ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa ni ya
kuvutia na kila timu ilicheza kwa kujituma huku Sergio Aguero kwa upande
wa Man City na Gareth Bale kwa upande wa Madrid wakionekana kuwa
tatizo.
Kinda
Kevin De Bruyne alizidi kuonyesha ni kati ya wachezaji hatari kabisa.
Hata hivyo mabeki Sergio Ramos na Pepe waliweza kumthibiti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni