TANAPA KUZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
Picha zote na Mahmoud Ahmad Arusha
…………………………………………………………..
Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
Shirika
la Hifadhi za Taifa TANAPA limejipanga kuzindua kampeni ya kitaifa ya
kufanya usafi mlima Kilimanjaro ambao unakusanya mapato ya shilingi
bilioni 60 kwa mwaka na kuajiri Watanzania laki 3.
Meneja
Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na Waandishi wa
Habari amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuboresha mazingira safi ya
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuinusuru na uchafuzi wa mazingira wa
kidunia (Global warming), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),
inatarajia kuzindua kampeni ya usafi wa mlima Kilimanjaro kesho ambayo
itadumu kwa siku kumi.
“Tumeamua
kufanya usafi katika mlima huo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi
za Rais John Pombe Magufuli katika kuweka mazingira katika hali ya
usafi hususan hifadhi za taifa” Alisema Shelutete
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Utalii Sirili Akko amesema kuwa mashirika
binafsi yaliyoko kwenye sekta ya utalii hayana budi kushiriki katika
kufanya usafi katika mlima huo wa kwanza kwa urefu barani Afrika na
wapili duniani.
Pia
ameitaka serikali kusimamia maagizo ya Ofisi Makamu wa Raisi Mazingira
kwa kupiga marufuku ya matumizi plastiki katika hifadhi za taifa ili
kuepuka kuchafua mazingira.
Mdau
wa Masuala ya Utalii ambaye ni Afisa Masoko wa Hoteli ya Kibo Palace
Jenipher Swai amesema kuwa wameungana na Tanapa kufanya usafi kwa kutoa
vifaa vya kufanyia usafi pamoja na kushiriki kupanda mlima huo katika
madhimisho ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa hoteli hiyo.
Jumla
ya Watalii 50000 hutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro na
kuchangia shilingi bilioni 60,kampeni ya kufanya usafi ya muda wa siku
10 itanza kesho ikiwashirikisha wapagazi,waongoza watalii na wadau wa
utalii ,kuhakikisha hali ya usafi katika hifadhi zetu zitasaidia kuvutia
watalii zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni