By Newsroom on April 28, 2016
Meneja
 wa Huduma za Masoko Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiongea na 
wanahabari wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati 
ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo na Mgahawa wa Samaki samaki. Kulia
 ni Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa Samaki samaki, Saum Wengert.
Meneja
 wa Huduma za Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Olivier 
Prentout (kushoto) akiwa na Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa wa Samaki
 samaki, Saum Wengert wakionyesha mkataba wa ushirikiano wa kibiashara 
waliosaini kati ya kampuni ya Tigo na Mgahawa huo kwa waandishi wa 
habari jana jijini Dar Es salaam.   
…………………………………………………………………………………………….
 Kampuni ya simu inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali ya Tigo 
Tanzania, leo imeingia   ubia na mgahawa ya Samaki Samaki  ambao 
ilianzishwa tangu  mwaka 2007  ukiwa na matawi matatu  yaliyopo Mlimani 
City, City Centre na Masaki Jijini Dar es salaam,  ambapo pande hizo 
mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja  kwa kuleta  bidhaa/huduma zao 
kwa wateja wa kila mmoja. Akitangaza ubia huyo jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout aliviambia
vyombo vya habari kuwa ushirikiano huo ni moja ya alama ambazo zinajenga imani kwamba wateja wa Tigo ambao sasa wanaweza kujitambulisha kupitia migahawa ya Samaki Samaki Tigo imeweka mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote ya
Samaki Samaki ili kuwawezesha wateja wake kufurahia intaneti ya kasi na ya haraka wakati wakila na kunywa kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula vinavyotokana na mazao ya baharini hapa nchini.“Tunaamini ushirikiano wetu utandelea kuonesha ni jinsi gani tumejikita kwenye kuboresha mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya
kidijitali na kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa wateja wetu, alisema Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez. Aidha Muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos alisema Samaki Samaki wanawafanyia kazi Watanzania na wameungana na Tigo ambayo ni kampuni ya simu inayooongoza kwa ubunifu nchini kuwapatia wateja wake kile ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu kwa jinsi huduma za Tigo zilivyo hususani uzoefu kwenye mtandao wa bure na wa kasi wa intaneti. Kwa ushirikiano huu tutawapatia wateja wetu miradi mingi mipya, maboresho pamoja na ofa. Kufanya kazi na Tigo sio kwamba kunahusu sisi kupata fedha tu, bali inahusu ni nini cha ziada tunachoweza kuwapatia wateja wetu na hali kadhalika ni kwa kiasi gani tunaweza kujifunza kufanya kazi pamoja na kampuni iliyo na uzoefu mkubwa na ya kimataifa.Tunaweza kuwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula vinavyotokan na mzao ya baharini, lakini tunapenda kufanya jambo zaidi kwa ajili ya wateja wetu. Huduma za Tigo zinazotarajiwa kuwepo kwenye migahawa ya Samaki Samaki ni pamoja huduma ya bure ya intaneti bila nyaya (WiFi), Tigo Pesa na Tigo Music.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni