MKUU WA WILAYA YA MOSHI ,NOVATUS MAKUNGA AAJIONEA ATHARI YA MAFURIKO
Mkuu
 wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu 
alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya 
kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya
 kujionea hali ya mafuriko.
Mkuu
 wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi
 ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Mtaalamau
 anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro 
Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi 
kabla ya ndege kuruka.
Mkuu
 wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa 
ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo
 lililo athirika kwa mafuriko.
Maeneo
 mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji 
vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya.
Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya.
Maashamba yamejaa maji ,
Maeneo
 mengine barabara hazipitiki hali inayochangia wananchi wanaoishi katika
 maeneo hayo kushindwa kupata huduma za kibinadamu.
Eneo la Mabogini pia liliathirika na mafuriko ingawa yalikuwa ni ya muda mfupi.
Sehemu ya mji wa Moshi unavyoonekana kwa juu.
 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 



















 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni