HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MNH- YAWEKA MIKAKATI KUHAKIKISHA WATOTO WANAOZALIWA NA MATATIZO YA KUTOSIKIA WANAPATIA MATIBABU.
Mtaalam
 wa masikio Fayaz Jaffer akitoa elimu kwa wazazi / walezi , jinsi ya 
kutunza kifaa kinachomsaidia mtoto mwenye matatizo ya kusikia kuweza 
kusikia na kuwasiliana. Mtaalam huyo ametoa elimu hiyo leo katika 
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- alipokuatana na wazazi ambao watoto 
wao walifanyiwa upasuaji nchini India na kuwekewa kifaa hicho.
Kaimu
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- Profesa 
Lawrence Museru akielezea mipango ya MNH katika kuhakikisha huduma hiyo 
inakuja kutolewa hapa MNH kwa siku zijazo 
Baadhi ya wazazi wakimsikiliza mtaalam wa Masikio Fayaz Jaffer leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH.
Kaimu
 Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru pamoja na Mtaala wa masikio 
Fayaz Jaffer wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto ambao 
walifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa maalum cha kuwasaidia kusikia ili
 kuweza kuwasiliana.
Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Museru ( katikati) akiwa na Mkuu wa 
Idara ya Masikio , Pua na Koo Daktari Edwin Liyombo ( kushoto ) na Fayaz
 Jaffer .
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Hospitali
 ya Taifa Muhimbili-MNH- imeweka mikakati ya kuhakikisha watoto 
wanaozaliwa na matatizo ya kutosikia wanapatia matibabu hayo katika 
Hospitali hiyo ili kuwawezesha watoto wengi wenye matatizo hayo kupata 
huduma hiyo kwa wakati.
Mikakati
 hiyo imeelezwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
 MNH Profesa Lawrence Museru wakati akizungumza na wazazi / walezi ambao
 walifika MNH kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao ambao wana
 matatizo ya kusikia sanjari na kupata maoni mbalimbali kutoka kwa 
wazazi hao.
Akifafanua
 Profesa Museru amesema kimsingi mahitaji ya matibabu hayo ni makubwa na
 upasuaji huo haufanyiki nchini  hivyo wagonjwa hutegemea matibabu hayo 
nje ya nchi na ambayo ni gharma kubwa .
“ 
Mpango uliopo sasa ni kuhakikisha huduma hiii inafika hapa MNH ili 
wagonjwa wenye matatizo hayo waweze kutibiwa hapa nchini kwasababu tuna 
wataalam wa kutosha , pia naamini hatua hiyo itawasaidaia wananchi wengi
 kupata  matibabu hayo ” amesema Profesa Museru.
Kwa 
upande wake Mkuu wa Idara ya Masikio ,Pua na Koo wa MNH  Daktari Edwin 
Liyombo amesema tayari dokezo limeandaliwa ili kuiomba serikali 
kuanzisha program maalum itakayowasaidia Madaktari kupata mafunzo pamoja
 na kupata vifaa tiba ili upasuaji huo uweze kufanyika hapa nchini.
Kwa  
mujibu wa Daktari Liyombo mgonjwa mmoja akipelekwa nchini India kwa 
ajili ya kufanyiwa upasuaji hugharimu kati ya Shilingi Milioni 85 hadi 
Milioni 100  lakini endapo matibabu hayo yatafanyika hapa nchini gharama
 itapungua kwa kiasi kikubwa.
Akizungumzia
 kuhusu utaratibu wa kukutana na wazazi  ambao watoto wao wana matatizo 
ya kusikia, Daktari Liyombo amesema utaratibu huo ni endelevu kwani una 
lenga kufuatilia maendeleo ya mtoto na kumuwezesha mzazi kupata ushauri 
wa kitaalam , leo zaidi ya wazazi 40 wamejitokeza MNH kwa ajili ya 
kukutana na watalaam .
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni