MJANE WA MWALIMU BABA WA TAIFA MAMA MARIA ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI LEO
Mama
 Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya 
Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,  akiwa na 
mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari 
wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam. 
Mama Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana 
mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka  mingi 
iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John 
Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina  la Mwalimu na siyo
 yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na 
nvijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa..
PICHA NA IKULU
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni