BIMA YA AFYA YA AAR YAADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI HOSPITALINI AMANA
Kampuni  ya Bima ya AAR  imetembelea 
Hospitali ya Amana iliyoko Ilala Dar es salaam na kutoa msaada wa 
vyandarau kwa wamama wajawazito katika kutimiza lengo la kupunguza 
uenezi  wa gonjwa la Malaria. 
Akiongea na wandishi Habari 
Hospitalini hapo, Afisa Mahusiano wa kampuni ya bima ya AAR, Bibi Amisa 
Juma alisesema, “Tukiwa kama wadau wa Afya Tanzania, ni jukum  letu 
katika jamii kuonyesha mfano wa kupambana  na maradhi mbalimbali ikiwemo
 hili Malaria. 
Hii imakua ni  utamaduni kwa kampuni 
ya Bima ya AAR kuadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa kushirikiani na 
Jamii katika shughuli mbali ikiwemo kuchangia kutoa elimu juu ya 
kujikinga na tiba pamoja na kuchangia matibabu kwa jamii tofauti ya 
Tanzania. Almalizia Bibi Amisa.
Wafanyakazi wa AAR walitembelea hodi ya kina na mama wajawazito na watoto na kutoa msaada huo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni