ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MAISARA.
Vikundi vya mazoezi vikiwa katika
 matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo 
yamefanyika kuanzia Mazizini Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia 
Maisara Mjini Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais wa 
Zanzibar Balozi Seif Ali Idi (katikati) akiongoza Matembezi ya hiari ya 
kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia mazizini 
na kumalizikia maisara mjini Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya 
Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kushoto yake ni katibu Mkuu Wizara ya 
Afya Dkt  Juma Malik Akili.
Vikundi mbalimbali vya Mazoezi 
vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maisara katika 
maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo yamefanyika  Mjini Unguja.
Vikundi mbalimbali vya Mazoezi 
vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maisara katika 
maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo yamefanyika  Mjini Unguja.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit 
Kombo (wa mwanzo ) akishiriki katika mchezo wa kuvuta  kamba kwenye 
maadhimisho hayo ambapo timu ya Baraza la Wawakilishi ilipambana na 
Wizara ya Afya ambapo  Afya ilipata ushindi. 
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit 
Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria 
Duniani ambayo yamefanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais wa 
Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Maadhimisho ya siku ya 
Malaria Duniani ambayo yamefanyika Maisara Mjini Unguja.kulia yake ni 
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na Kushoto yake ni Katibu 
Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
……………………………………………………………………………………………………
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi 
amewataka wananchi wa wanaosafiri mara kwa mara  kwa ajili ya harakati 
zao za maisha kuchukua vyandarua na kuvitumia wanapokuwa safarini ili 
kujikinga na maradhi ya Malaria.
Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani 
katika viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar, Balozi Seif alisema licha ya
 Zanzibar kuwa na kiwango cha chini ya asilimia moja cha Malaria, 
utafiti unaonyesha watu wanaogunduliwa kuugua maradhi hayo hivi sasa ni 
wale wenye utaratibu wa kusafiri nje ya Zanzibar.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa 
dhati kuimarisha afya za wananchi na itaendelea kuboresha huduma za afya
 sehemu zote na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.
Hata hivyo alisema wakati Zanzibar inajivunia mafanikio 
katika vita dhidi ya Malaria bado maradhi ya Kipindupindu yanaendelea 
kuwa tishio  kwa wananchi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na 
wataalamu wa afya.
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Juma Malik Akili alisema 
katika kumaliza Malaria kuanzia tarehe 25 mwezi huu watatoa vyandarua 
 760,000 vilivyotiwa dawa bure kwa wananchi katika Wilaya zote za 
Zanzibar.
Amewashauri wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kikamilifu kwani inaonekana kuwa ndio njia kubwa inayosaidia kukinga Malaria.
Katika maadhimisho hayo, wananchi na vikundi vya mazoezi 
wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais walifanya matembezi ya hiari 
yaliyoanza Mazizini, Wilaya ya Magharibi B na kumalizia viwanja vya 
Maisara, Mjini Zanzibar.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni