MBUNGE WA SUMWE, RICHARD NDASA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUOMBA RUSHWA.
NA SHARIFA MARIRA, Dar
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo
tarehe 1/4/2016 imemfikisha Mahakamani Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa
Mbunge wa Sumwe ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Mtaji na Uwekezaji kwa
kosa la kushawishi na kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni thelathini
(30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11
ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a) na (2).
![Richard Ndasa, Mbunge wa Sumve (CCM)](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_suAkMBo-QkaIu2k0eMh7HEOjycmUhSf1W-1xGNfZwXa-T_cTpuCzE8oGYNhZeH7XtqnlmfJ_ZF-juFCObRAJcrS-35gp5l0pp4DybFcE8eqGf60TPcNlPEjzeAJoHz3thwnk6FJH8bnCINbIuaqjxXJQ=s0-d) |
Mh Richard Ndassa akichangia hoja kwenye mkutano . |
Akiwa kama mjumbe wa Kamati ya Mtaji na Uwekezaji tarehe
13/3/2016 Mhe. Ndassa alimwomba rushwa ya shilingi Milioni 30 kutoka kwa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi J.
Mramba ili amsaidie kuwashawishi wajumbe wengine wa Kamati Mtaji na
Uwekezaji kupitisha bila kipingamizi taarifa ya TANESCO kwa mwaka
2015/2016.
Mbunge huyo amefunguliwa kesi namba 118/2016 na alisomewa
mashtaka hayo na Wakili wa TAKUKURU Dennis Lekayo akishirikiana na
Emmanuel Jacob katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius
Mchauro.
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kupata mdhamini
mmoja na kulipa shilingi milioni 10. Uchunguzi wa shauri hili bado
unaendelea na kesi hii itatajwa tena tarehe 18/4/2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni