NA RAYMOND URIO, Dar
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Annastazia Wambura ameipongeza timu ya soka la Wanawake, “Twiga Stars”
kwa kazi waliyoifanya kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa upande wa
wanawake yatakayo fanyika nchini Cameroon.
Pongezi hizo zimeenda kwa kikosi kizima kutokana na juhudi walizo onesha kwenye
mechi dhidi ya Zimbabwe hapa nchini, ile na marudiano kuwa ni juhudi nzuri ya
kutovunjika moyo kwenye kuipeperusha bendera ya nchini.
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura,akiwapongeza wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake nchini “Twiga Stars” kwa kiwango walichokionyesha katika mechi ya marudiano na timu ya Zimbabwe alipokutana nao katika ukumbi wa Idara ya Habri MAELEZO,Dar es Salaam, jana.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wanawake nchini (TWFA),Amina Karuna na Makamu mwenyekiti wa chama hicho,Rose Kisiwa. Picha na Raymond Urio
Akizungumza na waandishi wa Habari jana, jijini Dar es salaam Naibu Waziri Annastazia, alisema kuwa ni jambo zuri la kuipongeza timu yetu hasa ukiangalia ni mchango mkubwa waliionesha japo hatupo tena katika mashindano hayo ila kwa juhudi waliionesha ni muhimu sana kuwapongeza.
“ Wachezaji wetu wameonesha kazi nzuri katika mechi
labda kwakuwa tatizo ni kutokuwa imara sana kwa muda nah ii inatokana na
kutokuwa na Ligi zao.
“Nimepanga kuisadia timu hii kwa kutaka kuweza
kufika mabli na hata kuibua vipaji vingine na kusimamia vyema soka kwa upandea
wa wanawake,” alisema Annastia.
Hata hivyo
Annastazia alisema kuwa anawaomba wazazi wote nchini kutokuwa na imani za zamani
kutowapa fursa watoto wa kike kukuza kitu anachotaka hasa kwa upande wa mchezo
kama huu wa mpira wa miguu na kuamini ni wanaume pekee ndio wanaocheza,
Licha hivyo Meneja wa timu hiyo Furaha Francis,
alisema kuwa uongozi wa timu unamuomba Naibu huyo kupitia serikali hii
kusimamaia vyema swa la mpira wa miguu kwa upande wa wanawake kutokana na
kusahaulika tangia nyuma.
“ Tulipoenda Zimbabwe tumeona, serikali ipo mstari
wa mbele kuisimamaia timu yao na kujojali ni upande upi walionao, ila kwetu
kitu kama hiko hakipo na si jambo jema inatakiwa na sisi tupate kuona thamani
yetu iko wapi kwenye suala la soka” alisema Furaha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni