Waziri Jenista atoa ubani kwa wafiwa maafa ya kawe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagamaakitoa ubani kwa Gaudensia Deogratius aliyefiwa na watoto wawili na mume baada ya kufunikwa na kifusi Kawe Ukwamani Dar Es Salaam Aprili 9, 2016Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa mkono wa pole kwa mama wa marehemu Ephrahim Mangule (aliyefariki kwa kuangukiwa na kifusi Kawe) wakati wa msiba huo Kinondoni Dar es Salaam tarehe 9 Aprili, 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagamaakitoa salamu za pole kwa wafiwa waliopotelewa na ndugu 3 baada
ya mvua zilizonyesha Aprili 7, 2016 na kuangukiwa na nyumba Kawe Dar es
Salaam kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.
Raymond Mushi akizungumza na moja ya familia ya wafiwa walioangukiwa na
kifusi Kawe Dar es Salaam wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
alipowatembelea tarehe 9, Aprili, 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akiangalia chumba kilichoangukiwa na kifusi baada ya mvua kubwa
zilizonyesha Aprili 7, 2016 na kuua watu 5 wa familia moja Kawe Dar es
Salaam.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Uratibu,Ajira,kazi na watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama
amewatembelea wananchi waliopatwa na majanga ya kuangukiwa na kifusi
eneo la Kawe na kuwapa mkono wa pole.
Akiongea na moja ya familia zilizopatwa na
maafa hayo Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa ya tukio hilo na kwa vifo vilivyojitokeza na
kuahidi kutoa ushirikiano kwa familia ya wafiwa na waathirika wa tukio
hilo.
“Ndugu zangu tumekuja kushirikiana nayi
kwenye msiba huu mzito, ambao wenzetu wamepoteza karibu familia nzima
kutokana na haya maafa, poleni sana kwa msiba na Serikali ipo pamoja
nayi katika kipindi hiki kigumu.” Alisema Mhe Jenista.
`
Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa
wananchi kutoa ushirikiano wakati Serikali inapokuja kwa ajili ya
kujadili jinsi ya kutatua mambo yanayowezesha kuhatarisha maisha yao
hasa, tatizo la makazi yaliyopo mabondeni kwa ajili ya usalama wao na
familia zao katika kuzingatia suala la mipango miji ili kuepukana na
majanga kama haya.
Aidha kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi amesema kwa upande wake amesikitishwa na
tukio hilo na kuongeza kuwa Wilaya imejipanga kwa kushirikiana na
kamati ya maafa ya Wilaya na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili
kuendelea kuangalia ni kwa namna gani wataweza kuwasaidia wananchi
waliobaki katika maeneo hayo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya familia ya
wafiwa Bi Gaudencia Deogratius ambaye amepoteza mume na watoto wawili
ameishukuru Serikali kwa faraja aliyopata kutoka kwa Waziri na
hakutegemea kupata ugeni huo na ameiomba Serikali kuwasaidia wale
waliopo mabondeni ili kuepusha majanga mengine zaidi kutokea.
Tukio la hili la nyumba kuangiwa na kifusi
katika eneo la kawe Jijini Dar es Salaam lilitokea April 7 mwaka huu na
kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni